TIMU ya wanawake ya mchezo wa Kabadi KMKM imefanikiwa kuondoka na ushindi baada ya kuilaza timu ya Lumumba kwa kuvuna pointi 71- 19.
Mtanange huo ulipigwa wakati wa uzinduzi wa ligi ya kwanza ya mchezo wa kabaddi katika viwanja vya new Amaan Complex mjini Unguja na kuhudhuriwa na mashabiki wengi wa mchezo huo.
Katika kipindi cha mwanzo cha mchezo huo timu ya KMKM ilikua ikiongoza kwa pointi 47 na upande wa Lumumba ikiwa na pointi 7.
Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili timu zote mbili zilionekana kuongeza nguvu na kila mmoja kutamani kuondoka na ushindi wa mchezo huo.
Timu ya KMKM ilifanikiwa kuongeza pointi 24 katika dakika hizo na Lumumba kuongeza pointi nane na kuisababishia KMKM kuondoka na ushindi uwanjani hapo.
Wakati huohuo timu ya KMKM kwa upande wa wanaume nayo iliondoka na ushindi baada ya kuifunga Lumumba kwa pointi 61 -30
Wachezaji wa Kabadi timu ya KMKM walisema kuwazidi nguvu wapinzani wao kunatokana na kuuzowea mchezo huo na kuendelea kuufanyia mazoezi mara kwa mara huku timu ya Lumumba ikisema kuwa mchezo huo ulikua mgumu kwao kutokana na kutokuwa na mashirikiano na hofu iliyowatawala dhidi ya wapinzani wao na kuahidi kurekebisha kasoro zilizojitokeza ili kufanya vizuri katika michezo ijayo.
Michuano hiyo ya siku tano inakwenda sambamba na kauli mbiu " miaka minne ya Dk. Hussein kabadi inajieleza"
WACHEZAJI wa kabadi timu ya Lumumba wanawake waliovaa flana nyeusi wakipambana na mchezaji wa mchezo huo wa timu ya KMKM, katika mtanange ulipigwa wakati wa uzinduzi wa ligi ya kwanza ya mchezo wa kabadi katika viwanja vya new Amaan Complex mjini Unguja. (PICHA NA MPIGA PICHA WETU).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...