Na Oscar Assenga, Korogwe

Waziri wa maji Jumaa Aweso amesema kuwa mradi wa maji wa miji 28 unatekelezwa katika wilaya nne za mkoa Tanga unakwenda kumaliza kabisa changamoto ya ukosefu wa maji.

Hayo ameyasema hayo wilayani Korogwe wakati alipotembelea eneo la chanzo Cha maji Cha Tabora kilichopo katika Kijiji Mswaa kilichopo wilayani Korogwe.

Amesema kuwa mradi huo ambao unatarajiwa kutumia kiasi cha sh Bil 170 hadi kukamilika kwake unatarajiwa kunufaisha wananchi waliopo katika wilaya za Muheza, Pangani,Handeni na Korogwe .

"Mpaka Sasa mradi umeweza kufikia zaidi ya asilimia 60 hivyo niwaombe wakandarasi kuhakikisha mnakamilisha mradi huu Kwa wakati Ili wananchi waweze kunufaika"amesema Aweso.

Aidha Waziri Aweso amewataka wananchi wa Kata ya Mswaha kuwa walinzi wa miundombinu ya mradi huo ambao umegharimu fedha nyingi zaidi.

Awali wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali Kwa mradi huo ambao utaweza kuwaepusha na kuliwa na mamba.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...