Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye pia ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe anatarajiwa kuwa Mgeni maalumu katika mkutano wa 24 wa Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe unaotarajiwa kufanyika Kampasi kuu Morogoro Novemba 23, mwaka huu.
Akizungumza na timu ya ujumbe kutoka Chuo Kikuu Mzumbe ikiongozwa na Mkurugenzi wa Ukimataifishaji na Baraza la wahitimu wa chuo hicho Dkt. Lucy Massoi iliyofika ofisini kwake Lumumba jijini Dar es Salaam Novemba 2 , Balozi Dkt. Nchimbi amekipongeza chuo hicho kwa kuendelea kuratibu na kuwakutanisha pamoja Wahitimu kila mwaka.
Balozi Dkt.Nchimbi ameongeza kuwa tukio hilo ni muhimu sana kwa ustawi wa elimu nchini kwani Wahitimu wanapokutana pamoja kutokea maeneo tofauti ya kitaaluma na utendaji kunatoa fursa ya kubadilishana uzoefu na kutoa mrejesho wa mafunzo waliyopokea dhidi ya hali halisi iliyopo katika utendaji na hivyo kusaidia maboresho kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mitaala ya kufundishia na kuwahimiza Wahitimu wote kuhudhuria mkutano huo sambamba na kujiunga katika jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
“Nimepokea kwa heshima kubwa sana wito huu wa kuwa Mgeni maalum na ninaisubiri kwa shauku kubwa siku hii ili niweze kukutana na Wahitimu wenzangu, Walimu wangu walionifundisha na Wafanyakazi kwa ujumla kwani ikiwa sasa ninaonekana ni kiongozi bora basi watu watambue Chuo Kikuu Mzumbe kina mchango mkubwa sana kwa kuwa ndipo mahali nilitumia muda mwingi kutafuta elimu na tunapaswa kujivunia kwa sababu kinafanya kazi kubwa ya kuwaandaa viongozi wa umma kwani hata Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni zao la chuo hicho, alisisitiza.
Balozi Dkt. Nchimbi alijiunga na Chuo Kikuu Mzumbe mwaka 1994 aliposoma Stashahada ya Juu ya Utawala wa Umma (ADPA) kwa kilichokuwa Chuo cha Uongozi wa Maendeleo (IDM) Mzumbe. Mwaka 2001, alirejea tena chuoni hapo kusomea Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA), na baadaye Shahada ya Uzamivu (PhD) mwaka 2008 na kuhitimu mwaka 2011. Anatarajiwa kuwa Mgeni Maalum katika mkutano wa 24 wa Baraza la wahitimu wa chuo hicho mwaka 2024.
Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na timu ya Wajumbe kutoka Chuo Kikuu Mzumbe (haipo pichani) waliofika ofisini Lumumba jijini Dar es Salaam
Timu ya ujumbe kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Dkt.Nchimbi Lumumba Dar es Salaam
Balozi Dkt. Nchimbi akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Ukimataifaji na Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt.Lucy Massoi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...