Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Yusuph Mwenda akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.
Mkuu wa Chuo cha Chuo Kodi (ITA) Profesa Isaya Jairo akizungumza wakati wa mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA), yaliyofanyika leo Novemba 22, 2024 Dar es Salaam ambapo wahitimu 417 wa kozi mbalimbali wametunukiwa vyeti.
SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imesema itaendelea kushirikiana na Chuo cha Kodi katika kutoa mafunzo ya kodi na forodha ilikuongeza makusanyo ya kodi kwenye Taifa na pato kwa ujumla.
Imesema inajivunia mchango unaotolewa na Chuo hicho katika kutoa mafunzo ya Forodha na kodi kwa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA )na watanzania kwa ujumla kwani yana uhalisia na fursa ya kipekee nchini
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya ameyasema hayo leo Novemba 22, 2024 wakati akimuwakilisha Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katika Mahafali ya 17 ya Chuo cha kodi (ITA).
Jumla ya wahitimu 417 wamehitimu katika ngazi ya cheti cha uwakala wa Forodha cha Afrika mashariki (CFFPC), Cheti cha awali cha usimamizi wa Forodha na Kodi(CCTM), Stashahada ya usimamizi wa Forodha na Kodi(DCTM), Shahada ya usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) pamoja na Stashahada ya uzamili katika Kodi (PGDT).
"Chuo kijikite katika tafiti zitakazotoa changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi na forodha kwani mapendekezo mengi yanayotolewa na jamii yanakosa utafiti au vithibitisho hivyo kufanya mwendelezo wa mapendekezo kuongezeka kwani hatujakidhi na kufikia malengo wanayoyataka,"alisema Mwandumbya.
Amesema, serikali imekuwa ikitambua mchango mkubwa unaofanya na Chuo cha Kodi kwa kutoa mafunzo ili kuwezesha kuwa na watumishi waliobobea na mahili katika ukusanyaji mapato.
Amesema mchango unaofanya na Chuo cha Kodi pia unasaidia kuongeza makusanyo ya Mapato ya Serikali na kuleta uhalisia wa kiutendaji
Pia Mwandumbya amesisitiza Chuo kiendelea kutoa mafunzo ya viwango vya juu huku kikizingatia kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani ndipo dunia inapoelekea kwa sasa hasa katika matumizi ya akili mnemba.
Mwandumbya pia amewataka wahitimu kushiriki katika kukuza pato la Taifa kwa kukusanya kile kinachostahili na watu kulipa kile wanachotakiwa kulipa hasa katika biashara za mitandaoni ama kimataifa ili serikali ikamilishe miradi yake.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amesema baraza lililopo liendelee kufanya kazi kwa uweledi ili kufanikisha watumishi kupata elimu itakayowezesha kuongeza idadi ya walipa kodi kwa hiari na kuboresha miundombinu bora kwa maendeleo ya nchi.
"Dhamira ya Chuo cha Kodi ni kukifanya kuwa cha kimataifa chenye kutoa wahitimu wabobezi katika masuala ya Forodha na Kodi" amesema Mwenda
Naye, Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Isaya Jairo amesema Chuo kimetengeneza wataalamu wengi wa forodha na kodi kwenye misingi ya kujenga umahiri na kukuza uchumi wa Taifa pamoja na kutumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi na itasaidia wahitimu hao waendane na kasi ya teknolojia na forodha ya dunia ya sasa.
Amesema pia kimekuwa kikitumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi kwa sasa ambayo itawasaidia wahitimu hao kuendana na dunia ya sasa
Chuo hicho kimetunuku vyeti kwa wahitimu 417 wa kozi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2023/2024 huku idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 wametunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF),Wahitimu 28 wametunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM),
61 wametunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119 wametunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14 wametunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akiwakabidhi zawadi wahitimu waliofanya vizuri katika masomo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...