SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewataka wamiliki na wadau wa usafiri wa majini kuepuka usafirishaji holela wa mizigo na abiria katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kwa maslahi binafsi ili kuepuka ajali.

Afisa wa TASAC mkoa wa Mara, Nurdin Basekanganya ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea mialo ya uvuvi na usafirishaji eneo la Bunda kwa lengo la kutoa elimu ya usalama majini

Amesema kila chombo cha usafiri wa majini kilichokaguliwa na kuidhinishwa na TASAC kimepewa leseni yake kulingana na muundo na uwezo wake na hivo kubadilishia matumizi ya chombo cha majini huenda ikapelekea ajali.

"Niwasisitize wamiliki wote wa vyombo vya abiria, wasipakie abiria kuzidi uwezo, au wasibadilishe matumizi ya kubadilisha abiria wakapakia abiria, kwani ni kinyume na kanuni zetu za TASAC.

"Wahakikishe wanafuata utaratibu, kama ni chombo cha abiria kipakie abiria, kwa uwezo ambao tumekipatia leseni na kama ni mizigo basi kipakie mizigo, kwa uzito kulingana na leseni", amesema Basekanganya.

Amesema TASAC imejidhatiti kuimarisha usimamizi wa vyombo vyote vya majini katika kuangalia usalama na ubora wa vyombo vya maji na kuhakikisha elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya uokoaji.

"Endapo mtu yeyote anayemiliki chjombo cha majini atabainika kutotumia 'life jacket' (Boya Okozi) basi hatutosita kumuchukulia hatua kali za kisheria" amesema.

Aidha amewakumbusha wasafirishaji na wavuvi wanafanya shughuli zao katika ziwa Victoria wahahakikishe kabla ya kuondoka wanapata taarifa za hali ya hewa ili waweze kuwa na uhakika juu ya usalama wao majini.

Wadau mbalimbali wameipongeza TASAC kwa hatua wanazoendelea kuchukua na kuwataka wananchi kuzingatia kanuni na taratibu na kuepuka kuendesha shughuli zao kiholela.
Afisa wa TASAC mkoa wa Mara, Nurdin Basekanganya akizungumza katika mialo ya uvuvi na usafirishaji eneo la Bunda kwa lengo la kutoa elimu ya usalama majini.
Afisa wa TASAC mkoa wa Mara, Nurdin Basekanganya akizungumza katika mialo ya uvuvi na usafirishaji eneo la Bunda kwa lengo la kutoa elimu ya usalama majini.


Timu ya TASAC ikiangalia vyombo vya usafiri majini Bunda mkoani Mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...