KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinashiriki katika Mkutano wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabianchi nchini Baku Azerbaijan unaofanyika Novemba 11 hadi 22, 2024 wa kuhamasisha wawekezaji na sekta binafsi kuwekeza nchini Tanzania katika miradi inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Katika mkutano huo, Tanzania ilikua na eneo maalum la kujinadi, maarufu kama Tanzania House ambapo TIC ilitoa taarifa kwa Mheshimiwa Dkt. Phillip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipotembelea eneo hilo kuhusu mipango ya kuitangaza nchi na kunadi miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano huo.
TIC imefanya mazungumzo na kampuni mbalimbali zinazohusika na uwekezaji katika sekta zinazolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kampuni zinazojihusisha na maeneo yafuatayo
- Uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia teknolojia zisizoharibu mazingira.
- Viwanda vya uzalishaji.
- Kilimo endelevu.
- Miradi ya kaboni kred
- Huduma za kifedha kwa miradi inayokabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Hatua hizi zinaendana na jitihada za Tanzania za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kama ilivyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka na Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi ambao unalenga kuiwezesha Tanzania kuhimili na kushiriki katika jitihada za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa mtazamo wa kufikia maendeleo endelevu.
Kwa kuhamasisha uwekezaji katika sekta hizi, TIC inalenga kuchangia katika juhudi za kitaifa za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kukuza maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kuwa 10% ya miradi inayosajiliwa TIC ni inayohusu kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi.
Wadau mbalimbali wakipata uelewa katika banda la Tanzania ( TIC)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...