Mwenyekiti wa Chama ACT- Wazalendo Taifa Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba vijana katika mwaka wa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 wanajukumu na wajibu mkubwa wa kuungana ili kuleta mabadiliko na kuinusuru Zanzibar .
Mhe. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo huko katika viwanja vya Kibanda Maiti mjini Zanzibar alipohutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliondaliwa na Ngome ya Vijana wa ACT kuaga mwaka wa 2024 na kuukaribisha kwamba wa 2025 ambao ni wa uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Mhe. Othman amesema kwamba haki za Zanzibar zimekuwa zikiendelea kubanwa kwa kipindi kirefu jambo ambalo litaendelea iwapo vijana watashindwa kuungana kuleta mabadiliko ya uongozi wa kisiasa hapa Zanzibar utakaokuwa na uwezio na ujasiri wa kuzidai haki hizo.
Mhe. Othman amezitaja haki hizo kuwa ni pamoja na mgao wa fedha zinazotokana na mapato ya Muungano pamoja na fedha zilizotokana na hisa za kuanzishwa benk kuu ya Tanzania baada ya kuvunjika sarafu ya Afrika Mashariki ambapo Zanzibar ilikuwa mwanachama kamili lakini hisa zake zliingia kwenye uanzishwaji wa Benki hiyo.
Amefahamisha kwamba licha ya kutungwa sheria ya kuanzisha tume ya pamoja ya fedha ya mwaka 1996, ili kujua mambo ya muungano, mapato na matumizi ya muungano na kugawana baina ya pande mbili, lakini mambo mengi hayakutekelezwa na rais wa Zanzibar wa wakati huo hakuisaini shria hadi 2003 aliposaini Dk. Karume kwa kuakikisiwa utekelezaji wake.
Amefahamisha kwamba Zanzibar inapaswa kudai na kulipwa haki yake hiyo ambayo kiwango kikubwa cha fedha kwa kuwa ni madai ya muda mrefu jambo ambalo litaisaidia Zanzibar kuondokana na mfumo wa mikopo inayoendelea kufanyika hivi sasa.
Aidha Mhe. Othman amesema kwamba kwa muda mrefu Tanzania kulipaswa kuundwe chombo cha Muungano kinachotwa tume ya pamoja ya fedha ambayo ingetumika kutambua kiasi cha mapato na matumizi ya shughuli za muungano na mgaao unaoweza kufanyika kwa upande wa Zanzibar.
Hata hivyo, amesema kwamba kwa muda mrefu serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ndio yenye mamlaka ya kuunda chombo hicho imepuuza kufanya ivyo huku viongozi wa Zanibar wakibaki kimya na kuendelea na kazi yua mikopo mikubwa ambayo itaigharimu sana Zanzibar.
Akizungunzia suala la matukio ya watu kufariki kwenye mikono ya vyombo vya dola amesema kwamba suala hilpo halikubaliki na kwamba ni kukosekana kwa utu na thamani ya mwanadamu kupuuzwa kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria ya kuutoa uhai wa mtu mwengine.
Naye Makamu mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya chama cha ACT Taifa Nassor Maruhun amewataka vijana wa Zanzibar kutambua kwamba wao ndio wenye dhamana ya kuleta mabadiliko na kuwataka kuungana ili kutimiza dhamira ya mageuzi yanayohitajika Zanzibar.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Mansour Yousuf Himid amesema kwamba katika nchi yenye demokrsia ya kweli kipimo cha mtu ama kionozi kupendwa na wananchi ni kwenye sanduku la kura na kwamba wazanzibar wanaitaji serikali itakayowajibika kwa wananchi.
Mwisho
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar leo Jumapili Disemba 29. 2024 kupitia kitengo chake cha habari.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...