*Atangaza rasmi kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi ndani ya Chama

*Baadhi ya makada wasema ndio mtu sahihi kwa siasa za sasa nchini

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho katika uchaguzi ujao ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikishikiliwa na Freeman Mbowe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 12, 2024 Jijini Dar es Salaam, Lissu amesema kupitia nyazifa mbalimbali alizopitia ameshaona maeneo ambayo yanahitajika kutekebishwa akipata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

Amesema ameandika barua kwa Katibu Mkuu, kuondoa kusudio la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, na amewasilisha barua ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

“Wanachama wenzangu wa CHADEMA, Katika uongozi wangu kwenye nyazifa mbalimbali kwenye chama ninaamini nanyi wanachama mnaamini yakuwa ninasifa za kutosha kabisa ya kugombea nafasi ya juu kabisa na kuweza kuongoza vizuri kupitia chama hiki”. Amesema

Amesema Mwanachama wa CHADEMA au Mtu mwingine anayeona ajabu au anachukizwa au kukwazwa na uamuzi wake wa kutangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho, atakuwa hajui au hataki kuenzi urithi walioachiwa na Wazee wao, Edwin Mtei na Bob Makani, kuachiana madaraka ya Uongozi ndani ya Chama kwa njia ya Uchaguzi huru na wa haki.

Aidha Lissu amesema Chama kinahitaji mawazo mapya kupitia uongozi mpya ili Chama kiweze kukua na kutekeleza yale ambayo yanahitajika.

Wakati Lissu akitangaza kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa baadhi ya makada hicho ambao wamezungumza na Michuzi TV na Michuzi Blog wamesema wamefurahishwa na uamuzi huo kwa madai kwa Chama hicho kilipofikia kinahitaji mawazo,mipango na ushawishi kwa ajili ya kuhakikisha CHADEMA irudi kwenye uimara kama ilivyokuwa zamani.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...