Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Appolinary Kamuhabwa akitoa Hotuba yake katika Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili. (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 5, 2024.
Mkuu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof.David Mwakyusa  akihudhurisha wahitimu  katika Mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili. (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 5, 2024














Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
JUMLA ya wanafunzi 1,309 wamehitimu masomo katika Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS).

Miongoni mwa wanafunzi hao wanawake ni 461 sawa na asilimia 35 ya wahitimu wote.

Hata hivyo chuo kimesema bado kinaendelea na mpango wake wa kuwezesha wanafunzi wa kike kujiunga na chuo hicho ili kuwe na asilimia sawa kati ya wahitimu wa kike na kiume.

Makamu Mkuu wa MUHAS, Appolinary Kamuhabwa amesema hayo jana Disemba 5,2024 wakati wa mahafali ya 18 ya Chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema katika mwaka wa masomo 2024/2025 chuo kimedahili wanafunzi 235 huku walioomba na wenye sifa wakiwa 5,243 hivyo changamoto kubwa ya kinashindwa kudahili wanafunzi wengi ni kutokakana na kukosekana kwa miundombinu ya kufundishia.

"ongezeko la wanafunzi wanaohitaji kusoma katika programu mbalimbali za afya katika chuo kikuu chetu bado linaendelea kuwa changamoto kubwa katika udahili wa wanafunzi mfano katika mwaka wa masomo wa 2024/2025 kati ya waombaji wenye sifa za kujiunga na Muhas 5,243 waombaji 235 katika fani ya udaktari wa binadamu ndio waliopata nafasi sawa na asilimia 4.5 huku walibahatika kuchaguliwa kwenye fani ya ufamasia wakiwa 101 kati ya waombaji 4,842 wenye sifa za kujiunga sawa na asilimia 2", amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha MUHAS Dkt. Rehema Horera amesema mapato ya ndani ya chuo bado hayajafikia kiwango cha kutosha kuendesha shughuli za chuo kwa ufanisi bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Amesema katika kulifanya hilo, chuo kimebuni miradi ya kuongeza rasilimali fedha ambapo katika mwaka huu Chuo kimepitisha mpango wa kuzalisha pesa ( MUHAS Business Development Plan) ili kuweza kujiendesha.

"Lengo kubwa la mikakati hii ni kuongeza upatikanaji wa fedha ili kuboresha maslahi ya watumishi, Miundombinu ya kufundushia na kujifunza, tafiti, bunifu na shughuli za utawala.

Aidha Dkt. Horera amesema, February 29, 2025 chuo kitafanya kongamano la kumuenzi aliyekuwa Mkuu wa Kwanza wa chuo hicho Hayati Dkt. Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki dunia Mei 29, 2024 kwa kwa mchango mkubwa aliotoa kwa maendeleo ya MUHAS.

"Maandalizi ya kongamano hilo maalamu la kuadhimisha mwaka mmoja wa maisha ya Dkt. Mwinyi yameanza, kongamano hili muhimu litafanyika Februari 29,2025 na litakuwa linafanyika kila mwaka Mwezi Mei ambao ndio mwezi aliozaliwa Dkt. Mwinyi".

Amesema kwa kuwa Dkt. Mwinyi alikuwa mfano bora wa kuigwa kwa kushiriki mazoezi ya mwili basi makongamano hayo yatajikita kwenye magonjwa yasiyoambukiza ili kuenzi na kuchochea mabadiliko ya tabia zinazosababisha ongezeko la magonjwa hayo.

Naye, Satrumin Shirima, mwakilishi wa wahitimu wa shahada za Awali, amewashukuru wahadhiri na washauri kwa msaada na mwongozo waliowapatia muda wote wa mafunzo yao kwani kujitoa kwao kumewapa moyo na kuwajenga vema ndani yao na hata kwa familia na jamii.

Amesema watatumia changamato watakazokutana nazo kwenye ulimwengu wa kitaalamu kama fursa ya kukua zaidi ili wawena ujasiri na umilivu huku wakijua kuwa kila kikwazo kinaweza kuwapeleka kwenye mafanikio zaidi.

"Tunapaswa kukumbuka kuwa mahafali haya siyo mwisho bali ni mwanzo, jukwaa la kuingia kwenye mustakabali uliojaa fursa, tukafanye mabadiliko chanya katika dunia inayotuzunguka na tutumie mafunzo tuliyoopata kuleta tofauti kwenye maisha ya wengine."Amesema

Mwakilishi wa Wahitimu wa Shahada za Uzamili, Katunzi Mutalemwa amewaomba wahitimu wenzake kutumia ujuzi na umahiri walioupata wakati wa masomo ili kutoa huduma nzuri na bora kwa jamii.

'Ninaomba tujipe changamoto ya kuwa na ndoto kubwa zaidi ya 8 kwani hapa ni mwanzo wa Safari ya kufika umahiri wa juu wa afya hivyo nawahimiza wahitimu wenzangu tusiishie hapa bali huu uwe mwanzo wa kusonga mbele." Amesema Mutalemwa.

Katika mahafali hayo wahitimu 119,wametunikiwa Stashahada na Stashahada ya juu katika fani mbalimbali za afya na Sayansi shirikishi,Pia wahitimu 708 wametunukiwa Stashahada ya kwanza , na wengine 441 wakitunukiwa Shahada ya uzamili na wahitimu 33 wakitunukiwa shahada za uzamili za ubobezi lakini kipekee wapo wahitimu wawili waliotunukiwa shahada katika program mpya ya shahada ya uzamili ya ubobezi kwenye uchunguzi wa magonjwa ya wanawake kwa kiradiojia.

Aidha wahitimu nane wametunukiwa Shahada ya uzamivu ya Udaktari wa falsafa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...