Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katikati, Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendele la Kimataifa la Ufaransa(AFD), Celine Robart, na kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa hapa nchini Tanzania, Axel-David Guuillon wakionesha mikataba ambayo imesainiwa leo Desemba 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI ya Tanzania imesaini mikataba minne yenye thamani ya Uro milioni 118.8 ambayo ni sawa na shilingi bilioni 323.4 na Shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinaendelea kufanyika hapa nchini.
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza leo Desemba 06,2024 jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini mikataba hiyo, amesema kuwa mikataba hiyo inahusisha nishati jadidifu pamoja na utunzaji wa hifadhi ya mikoko.
Akichambua Mikataba hiyo Dkt. Mwigulu amesema mkataba wa kwanza ni mkopo nafuu wa Uro milioni 75.9 kwaajili ya mradi wa nishati ya jua wa awamu ya pili ambayo itatekelezwa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga na unatarajiwa kuzalisha megawati 100 ambapo itafanya kuwa na jumla ya megawati 150.
Ikiwa ni mwendelezo wa mradi wa kwanza wa uzalishaji nishati ya jua ambao ulisainiwa Juni 11, 2021 na tayari utekelezaji wake unaendele ambapo matarajio yake ilikuwa ni kuzalisha megawati 50 utakapokuwa umekamilika.
Dkt. Mwigulu amesema...."mkataba tuliosaini leo Desemba 06, 2024 utakuwa wa awamu ya pili ambao ni mhimu kwa sababu utaweza kutengenezea mradi utakaozalisha megawati 100 na hivyo kufanya jumla kuu megawati 150."
Mkataba wa pili ni wa mkopo nafuu wa Uro milioni 39.9 kwa ajili ya mradi wa uendelezaji wa misitu na utunzaji wa hifadhi ya misitu ya mikoko.
Amesema mkataba wa tatu ni wa msaada wa Uro milioni mbili ambazo ni maalumu kwa ajili ya utunzaji wa hifadhi ya mikoko huku mkataba wanne ukiwa ni wa msaada wa Uro Milioni moja kwa ajili ya kufadhiri mpango kazi wa kijinsia wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Mradi wa uendelezaji wa nishati ya jua.
"Haya ni maeneo makubwa ambayo yamehusisha mikataba ambayo tumeisaini ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa dira ya Taifa na maono ya Mh. Rais Dkt. Samia katika kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinafanyika kwa ukamilifu." Amesema Dkt. Mchemba
Kwa upande wa Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema kuwa mikataba iliyosainiwa leo Desemba 06, 2024 utaenda kusaidia katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia jua, mradi ambao utaenda kuzalisha megawati 150, ambao ni mradi mhimu katika kuchagiza nishati jadidifu.
"Mtazamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha tunavyo vyanzo vya umeme ambavyo ni nishati jadidifu ambavyo kwa kiasi kikubwa vinachangia kupunguza athari katika mazingira." Amesema
Amesema Mradi Sola wa Kishapu ulishaanza ambao unatekelezeka umeshaanza kuzalisha megawati 50 za kwanza na awamu ya pili kwa mega wati 100 ambapo inafanya kuwa na megawati 150 na fedha ambazo zimesainiwa leo ni kwaajili ya utekelezaji wa mradi awamu ya pili wa sola.
"Sisi tunafurahia sana kwa sababu ukiangalia vyanzo vyetu vya nishati ambavyo vipo kwa Tanzania karibia asilimia 58 ya vyanzo vya nishati ni Maji, asilimia 38 tunatumia gesi na asilimia chache tunatumia mafuta ya Dizeli na biogasi." Amesema Judith
Akizungumzia upande wa Utalii, Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Dunstan Kitandula amesema, Tanzania kuna hekta zaidi ya laki tano (500,000) uhitaji wa kupanda miti bado ni mkubwa kwa hiyo fedha hizo zitakwenda kusaidia kupanda miti kwenye mashamba ya Serikali yanayosimamiwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika shamba ya Silayo na Shamba la Songea.
Ameingeza kuwa kuna umhimu wa kutunza miti aina ya Mikoko hivyo fedha hizo zitaenda kusaidia kuimarisha usimamiaji wa misitu ya mikoko ambayo inafyonza kwa kiasi kikubwa hewa ya ukaa pamoja na kuzuia mmomonyoko baharini na ni muhimu kwa watu wa Pwani pia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katikati, Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendele la Kimataifa la Ufaransa(AFD), Celine Robart, na kulia ni Naibu Balozi wa Ufaransa hapa nchini Tanzania, Axel-David Guuillon wakiasaini mikataba mnne kwaajili ya nishati jadidifu pamoja na utunzaji wa mikoko pamoja na upandaji wa miti katika mashamba ya serikali. Mikataba hiyo imesainiwa leo Desemba 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katikati akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendele la Kimataifa la Ufaransa(AFD), Celine Robart wakibadilishana mikataba kusaidia kuhifadhi misitu ya mikoko, Kupanda miti, kuzalisha nishati ya jua pamoja kufadhiri mpango kazi wa jinsia wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Mradi wa uendelezaji wa nishati ya jua.
Mikataba hiyo imesainiwa leo Desemba 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba katikati akibadilishana mkataba Naibu Balozi wa Ufaransa hapa nchini Tanzania, Axel-David Guuillon wakibadilishana mikataba kusaidia kuhifadhi misitu ya mikoko, Kupanda miti, kuzalisha nishati ya jua pamoja kufadhiri mpango kazi wa jinsia wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Mradi wa uendelezaji wa nishati ya jua. Mikataba hiyo imesainiwa leo Desemba 06, 2024 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza jijini Dar es Salaam leo Desemba 06, 2024 mara baada ya kuasaini mikataba mnne kwaajili ya nishati jadidifu pamoja na utunzaji wa mikoko pamoja na upandaji wa miti katika mashamba ya serikali.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...