DAR ES SALAAM – Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imetangaza nafasi 59 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ufanisi wa uendeshaji na kuendana na kasi ya upanuzi wa huduma zake.

Nafasi hizi zinahusisha idara mbalimbali, ikiwemo Uendeshaji wa Ndege, Upangaji wa Ratiba za Wahudumu, Mauzo na Masoko, Usaidizi wa Rampu, na Udereva, kwa lengo la kuongeza nguvu kazi inayohitajika katika kipindi hiki cha ukuaji wa ATCL.

Nafasi za ajira zilizotangazwa ni:

✈ Afisa Uendeshaji wa Ndege (5) – Wenye leseni ya Flight Dispatcher kutoka TCAA au ICAO.

✈ Afisa Upangaji wa Ratiba za Wahudumu wa Ndege (2) – Wenye Shahada na cheti cha usafiri wa anga.

✈ Madereva (37) – Wenye Cheti cha Kidato cha Nne, leseni ya daraja C1 au E, na uzoefu wa mwaka mmoja.

✈ Afisa Mauzo na Masoko Msaidizi (1)

✈ Afisa Mauzo na Masoko (2) – Wenye Shahada na cheti cha masuala ya anga, kama Cheti cha Usimamizi wa Huduma za Ndege.

✈ Msaidizi wa Rampu (12) – Wenye Cheti cha Elimu ya Sekondari na cheti cha masuala ya anga.

Hii ni fursa muhimu kwa wale wanaohitaji kuwa sehemu ya Kampuni hii inayoendelea kukua kwa kasi kwa kutanua mtandao wake wa safari za ndani na kimataifa.

Aidha, Waombaji wenye sifa watapaswa kutuma maombi kupitia link ya ajira iliyo kwenye tovuti ya ATCL:https://www.airtanzania.co.tz/careers ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa tangazo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...