*Mabindia Hemed na Paul kushuka katika pambano usiku wa Valentin Day.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Umoja wa Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda Mabibo Mwisho (BMM) umesema kuwa Serikali imeweka kipaumbele cha michezo katika kuwainua vijana kujiajiri ambapo BMM inakwenda kutoa mchango wake kwa vijana kwenye ngumi kwa kutoa ufadhili na usimamizi wa vijana hao.
Vijana wa michezo ya ngumi wanatakiwa kuungwa mkono katika vipaji vyao katika kuweza kuwa na ajira ambayo ni mchezo wa ngumi na kufika mbali ya matarajio yao.
Akizungumza na Michuzi Media Mabibo Mwisho Mwenyekiti wa (BMM) Hamis Mwela amesema wakati sasa umefika kusaidia wengine ambao ni mabondia kuwafadhili katika kazi hiyo kutokana na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kaonyesha uungwana kwa vitendo katika sekta ya michezo.
Mwera amesema kuwa wanamuarika Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari ,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Greyson Msigwa kushuhudia BMM walivyodhamiria katika kuunga mkono Serikali katika mchezo wa Ngumi.
Amesema Vijana kujiajiri katika mchezo wa ngumi ni fursa ya kwenda kutatua ajira kwa vijana wenye vipaji.
Katika kufanikisha adhima ya kuwa na mapambano wameandaa usiku wa Nguumi Febraruari 14 katika ukumbi wa Bar Village Ubungo Maziwa.
Nae Katibu wa BMM Ramadhan Said amesema katika utaratibu wao wa kuchangishana wameweza kuwa na fedha ya kuwafadhili mabondia wawili kuingia nao mikataba ambao ni Paul Magesta pamoja na Hemed Rashid huku BMM ikiwa inahitaji mabondia wengine.
Amesema kuwa mabondia hao watasimamia katika mazoezi yao pamoja na masuala mengine katika maisha yanayoendelea ya kila siku.
Amesema katika usiku wa ngumi wa Februari 14 wameweza kupata ushirikiano na baadhi ya wadau kudhamini ngumi hizo.
Amesema kuwa katika umoja wao kumekuwa na mwitikio katika udhamini huo kwani unatokana na michango yao ya kila siku.
Aidha amesema kuwa watashirikiana na mabindia hao katika mapambano ambapo mapromota wakiwahitaji katika mapambano wawasiliane na BMM.
Hata hivyo amesema kuwa wananchokitoa kwa sasa ni kuwainua vijana wenzao katika ubondia na wao waje kurudisha kwa makundi mengine.
Bondia Paul Magesta amesema kuwa anashukuru udhamini wa BMM na kuahidi kufanya kazi ya ubondia kwa ufanisi katika mapambano akayokutana nayo ikiwemo pambano la Februari 14 la Usiku wa Wapendanao
Kwa upande wa Rashid Hemed Rashid amesema yuko tayari kwa kazi yeyote ya ubondia kutokana na kupata ufadhamini na ufadhili kwa BMM kuoyesha uwezo wake katika pambano litalofanyika Februari 14.
Amesema katika kipindi kirefu alikuwa hajapata mdhamini na mfadhili na kufanya kazi yake kuwa ngumu ikiwemo kulipa gharama za mazoezi lakini usimamizi wa BMM kazi imekuwa nyepesi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Usafairishaji Mabibo Mwisho (BMM) Hamis Mwela Akizungumza kuhusiana na BMM kuwasimamia mabondia wataopambana Usiku wa Valentine Day Village Bar Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wadhamini wa Ngumi Mkurugenzi wa Madson Joephat James akizungumza kuhusiana udhamini wa ngumi usiku Valentine Day zinazosimamiwa na BMM zitazofanyika Village Bar Ubungo jijini Dar es Salaam. Wadhamini wa Ngumi Tatu Shaban akizungumza kuhusiana na udhamini wa ngumi usiku Valentine Day zinazosimamiwa na BMM zitazofanyika Village Bar Ubungo jijini Dar es Salaam.
BMM wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza kuhusiana mabondia kuzichapa usiku wa Valentine Day jijini Dar es Salaam .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...