Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Juliana Masabo, ameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kwa juhudi zake kubwa katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya dawa za kulevya.

Akizungumza wakati alipotembelea banda la Mamlaka katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria mkoani Dodoma, Mhe. Masabo alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuelimisha jamii, hasa wanafunzi, ambayo kwa sasa wako kwenye hatari ya kuingizwa kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Aidha, Mhe. Masabo ametoa wito kwa Mamlaka kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuweka mikakati kabambe inayolenga kuelimisha na kuwakinga wananchi dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Kadhalika, alisisitiza kuwa elimu ni silaha muhimu katika kupambana na tatizo hili na kwamba ni muhimu kwa Mamlaka kuongeza nguvu katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...