NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TUNDU Lissu ameibuka mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) dhidi ya mpinzani wake ambaye mtangulizi wake, Freeman Mbowe aliyekuwa anatetea nafasi yake.

Katika ukurasa wake wa Mtandao kijamii wa X, Mbowe ameandika ujumbe wa kukubali kushindwa kwa kusema "Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya Uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama",

Mbowe ameikiongoza Chama tangu alipochaguliwa nafasi hiyo mwaka 2004 akirithi mikoba ya Bob Makani aliyeongoza chama hicho kuanzia mwaka 1999. Tundu Lissu nae amekuwa kwenye Chama hicho kwa zaidi ya miaka 20 huku akishika nafsi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama ambapo kabla ya uchaguzi huu alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...