NA BELINDA JOSEPH, RUVUMA.
Mbunge wa Jimbo la Madaba Mhe Joseph Kizito Mhagama, ameeleza mafanikio yaliyofanyika kwenye sekta afya katika Kata ya Mtyangimbole, kufuatia kuwepo kwa ongezeko la watu wamefanikiwa kujenga Kituo cha afya ambacho kinafanana na hospital ili kuondoa adha ya upatikanaji wa huduma hiyo ambayo hapo awali walikuwa wakitibiwa kupitia zahanati ya Misheni.
Akiwa katika ziara ya kikazi ya kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi kwa miaka Minne na kupokea changamoto kwa kila Kijiji ndani ya Jimbo la Madaba Mhe. Mhagama amefika katika Kata ya Mtyangimbole ambapo amewataka wananchi kuwaonyesha kwa vitendo wale ambao watahoji kuhusiana na utekelezaji wa ahadi mbalimbali alizozitoa pamoja na mafanikio ya Jimbo hilo wasisite kuwapandisha usafiri wapikipiki yaani bodaboda nakwenda kuwaonyesha kila jambo lililotekelezwa.
Amefafanua kuwa tangu nchi ilivyopata uhuru eneo hilo halikuwahi kujengwa Kituo cha afya, kipekee ametoa pongezi na shukrani zake kwa Kanisa la Katoliki kwa kuwezesha jamii ya eneo hilo kwa miaka mingi kupata huduma za kimatibabu kutokana na kutokuwepo kwa huduma hiyo kwa kipindi cha nyuma lakini katika uongozi wake kwenye Jimbo la Madaba Serikali imeweza kujenga kituo hicho.
Amebainisha kuwa kwa kushirikiana na Diwani wa kata hiyo pamoja na viongozi wengine wameweza kupita na kukagua maeneo yote kwa pamoja na kubaini changamoto mbalimbali ameahidi kwenda kuhakikisha zinatatuliwa kwa wakati pamoja na ujenzi wa wodi kwenye kituo hicho cha afya.
Wakizungumza baadhi ya kinamama waliokuwa katika eneo hilo wamempongeza Mbunge huyo kwa kuweza kutambua changamoto zao ikiwemo huduma ya Mama na mtoto na kutoa kipaumbele katika ujenzi wa kituo cha afya jambo ambalo limesaidia kuboresha huduma hizo kwa kuokoa vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua pamoja nakurahisisha gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda maeneo ya mijini kupata huduma bora ambayo kwa sasa wanaipata moja kwa moja kwenye kata hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...