Na Yeremias Ngerangera.....Namtumbo
Mama Mmoja aitwaye Mwajibu ALifa (58) Mkazi wa kitongoji Cha Muungano katika Kijiji Cha Mtonya Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma alikamatwa na mamba siku ya jumapili katika mto Luegu alipoenda kuchota maji ya kunywa na Kisha kutokomea Naye ndani ya maji .
Diwani wa kata ya Likuyu Kassimu Gunda alisema msako wa wananchi wa kitongoji Cha Muungano katika Kijiji Cha Mtonya na wananchi wengine wa Kijiji hicho waliziba mto Kwa miti ili kumfanya mamba asitoroke na mwili wa marehemu lakini Pamoja na jitihada hizo wananchi Kwa usiku kucha walimtafuta mamba na mwili wa marehemu Bila mafanikio.
.
Gunda alidai wananchi wa Kijiji hicho Cha Mtonya Bado wanaendelea na msako siku ya pili ili kuhakikisha wanamtafuta mamba huyo usiku na mchana .
Mwenyekiti wa kitongoji Cha Muungano Amiri Selemani Simba alidai marehemu alikamatwa na mamba akiwa na mjukuu wake ambapo baada ya kukamatwa na mamba huyo mjukuu wake alilia kumwona bibi yake akitokomea na kwenda kutoa taarifa Kwa wananchi huku akibubujika Kwa machozi.
Wananchi walielekea eneo la tukio na Hatua ya kwanza walilizingira Lile eneo na kuziba mto Kwa miti ili yule mamba asiende mbali na Lile bwawa alilimkamatia marehemu Mwajibu.
Hata hivyo wananchi walikesha usiku kucha kumsaka mamba huyo katika Lile eneo alilokamatiwa marehemu Bila mafanikio yoteyote.
Mtendaji wa Kijiji Cha Mtonya Maria Gerewadi Mbawala Pamoja na kukiri kutokea Kwa tukio Hilo aliwataka wananchi nyakati hizi za masika kujiepusha kuchota,kuoga ,kuvuka kwenye maji katika mto Luegu Kwa kuwa mto huo una mamba wengi na hataraishi Kwa maisha ya binadamu.
Afisa maliasili ,utalii na utunzaji wa mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Prisca Msuha yupo katika eneo la tukio kushirikiana na wananchi kumtafuta mamba huyo Pamoja na mwili wa marehemu
Mto Luegu uanaoanzia katika Kijiji Cha Ngwinde Wilayani Namtumbo umekuwa na mamba wengi nyakati za masika na husababisha watu kukamatwa na kuliwa na mamba hao Kila mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...