KAMATI ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi, Mawasiliano, Ardhi na Nishati Zanzibar, imelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa utendaji kazi madhubuti katika usimamizi wa bandari na bandari kavu hapa nchini pamoja na usimamizi wa sheria na kanuni za usalama, ulinzi na utunzaji mazingira wa usafiri majini.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Yahya Rashida Abdulla, leo tarehe 03 Februari 2025, walipotembelea Ofisi za TASAC mkoani Tanga na kufanya kikao na watumishi wa TASAC pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na kupongeza utendaji kazi katika Bandari hiyo na kupata matokeo chanya yenye maslahi mapana kwa Taifa.

"Tumefurahishwa na utendaji kazi mzuri wa TASAC katika udhibiti na usimamizi wa safari kwa njia ya maji hasa katika Bandari hii ya Tanga ambayo kwa kiasi kikubwa imerahisisha usafiri kati ya Tanzania Bara na Visiwani kwa eneo hili la mwambao ambalo lilikua na changamoto kubwa ya usafiri kwa njia ya maji,” amesema Mhe. Abdulla.

Aidha, Mhe. Abdulla ameongeza kuwa mafanikio haya ni makubwa kwani kwa sasa meli zinaweza kutoka Tanga hadi Zanzibar bila kupitia Dar es Salaam.

“Nimefurahishwa sana kuona sasa abiria wanaweza kufanya safari toka Zanzibar kuja Tanga bila kupitia Dar es Salaam, kwa hakika ni mafanikio makubwa sana. Hivyo niwapongeze sana kwa hatua hizi zilizopigwa na mamlaka hizi mbili TASAC na TPA," ameongeza Mhe. Abdulla.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TASAC, Meneja Mafunzo na Utoaji vyeti Mha. Lameck Sondo ameishukuru Kamati hiyo na kuahidi kuendeleza weledi, ufanisi na mashirikiano katika kudhibiti shughuli za usafiri majini kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mha. Sondo ameongeza kuwa TASAC inaendelea na utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa usalama wa usafiri katika Ziwa Victoria (Multinational Lake Victoria Maritime Communications and Transport (MLVMCT) project) ambao ni mradi wa ushirikishwaji wa nchi za Uganda na Tanzania katika kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mha. Sondo amesema kuwa Serikali kupitia TASAC imeendelea na ujenzi wa kituo kikuu cha uratibu wa masuala ya Utafutaji na Uokozi (Maritime Rescue Cordination Centre – MRCC) katika Ziwa Victoria ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 67.

Aidha, ameelezea kufanikiwa kwa hali ya juu katika ukaguzi wa meli za kigeni, pamoja na kutoa mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajengea uwezo watumishi wake katika kutekeleza majukumu hayo ya kiudhibiti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...