Na Humphrey Shao .


Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam imekwishaanza kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za DMDP awamu ya pili katika Wilaya zote za Ubungo ,Ilala, Kinondoni , Temeke na Kigamboni.

Hayo yamethibitishwa na Meneja Tarura Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa barabara cha mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya DMDP umekwishaanza na baadhi ya wakandarasi wapo saiti.

" Miradi ya DMDP iliyosainiwa imekwishaanza toka tarehe 15 mwezi Januari mwaka huu na sasa hivi wakandarasi wote wako ‘site’ wanafanya kazi za awali za uondoaji miuondombinu ya Tanesco na Dawasa ili mradi ukianza kusiwe na usumbufu" amesema Mhandisi Mkinga.

“Hatua nyingi za awali za kimikataba zimefika mwisho sasa tumeingia katika utekelezaji hivyo ni jambo la lazima kuondoa miundombinu mingine ili tuweze kuweka mitambo barabarani”.Aliongeza

Hata hivyo ametaja kuanza kwa ukarabati wa maeneo ambayo yaliathiriwa na mvua za El Nino pamoja na utekelezaji wa miradi midogo midogo katika mkoa















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...