Vodacom imezindua duka jipya katika eneo la Bombambili Manispaa ya Songea March 17, 2025, litakalosaidia wakazi wa eneo hilo kupata huduma bora na za uhakika kwa urahisi zaidi, Hili ni duka la pili katika Manispaa ya Songea, linalolenga kufanikisha huduma kwa wateja wengi zaidi.



Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye hafla hiyo Joseph Martin Kabalo, ambaye ni Afisa Biashara wa Mkoa huo, amepongeza uwepo wa duka hilo akisema kuwa utasaidia wakulima na wafanyabiashara kupata huduma bora zinazoweza kuleta manufaa makubwa.


Akitaja changamoto zinazowakumba wafanyabiashara wa mazao wanaofuata maeneo ya vijijini, Kabalo amesema kuwa tatizo kubwa linatokana na upungufu wa mtandao, jambo linalowafanya wafanye miamala ya simu kwa ugumu au kushindwa kuwasiliana na wateja wao ambapo Amewataka Vodacom kuongeza wigo wa huduma ili kufanikisha wananchi wa maeneo hayo kunufaika na mtandao.



Kabalo ameongeza kuwa Songea ni mji unaokua kwa kasi kimaendeleo, Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Mkoa wa Ruvuma una idadi ya watu milioni 1.848. "Uwepo wa huduma bora za mawasiliano utaimarisha na kuongeza chachu ya maendeleo ya kiuchumi," alisema Kabalo.


Meneja wa Vodacom Kanda ya Kusini Abednego Mhagama, amesema Wamegundua watanzania wengi wanahitaji huduma bora za mawasiliano, ambazo kimsingi zinatolewa na Vodacom pekee na kufuatia uwepo wa duka hilo, utawasaidia wateja wengi kupata huduma ambapo wamefanikiwa kutoa ajira kwa maelfu ya wananchi pamoja na fursa nyingi zinazotokana na uwepo wa mtandao huo hivyo kwa kutambua hilo wameamua kusogeza huduma karibu ambayo itasaidia wajasiriamali na wafanyabishara kunufaika zaidi.


Kwa upande wa wateja  wa mtandao wa vodacom Sarah Onesmo na Naj Mhelela, wamefurahishwa na Vodacom kuamua kufikisha huduma hiyo kwenye eneo lao kwani kupitia halfla ya uzinduzi wa duka hilo wamepata elimu ya matumizi sahihi ya mtandao wa vodacom huku wakiwapongeza kwa kuamua kusogeza huduma kwani hapo awali walilazimika kutumia nauli kwenda mjini kufuata huduma nakutoa rai kwa wananchi wengine kwenda kupata huduma ili wanufaike na ofa mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...