Zoezi la kulishana Keki wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA
Zoezi la kukata Keki wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA


Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wanawake na Wasichana wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) wamezindua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani 2025, yakiongozwa na kauli mbiu "Wanawake na Wasichana 2025: Haki, Usawa na Uwezeshaji katika Sekta ya Maji".

Maadhimisho haya yanalenga kuhamasisha na kuonyesha umuhimu wa haki na usawa wa kijinsia katika upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za maji.

Uzinduzi huo umefanyika leo, Jumatatu Machi 3, 2025, na umetanguliwa na zoezi la usafi wa mazingira katika ofisi za SHUWASA, ambapo wafanyakazi wanawake wa SHUWASA pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Town wameshiriki kwa pamoja katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi, amesema ni muhimu wanawake kuwezeshwa katika sekta ya maji ili waweze kuchangia kikamilifu katika usimamizi wa rasilimali hizi muhimu.

“Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu ni fursa muhimu sana ya kutambua na kusherehekea mchango mkubwa wa wanawake na wasichana katika jamii zetu na kusisitiza umuhimu wa haki na usawa wa kijinsia katika upatikanaji na usimamizi wa rasilimali za maji",amesema Jilumbi.

Ameongeza kuwa wanawake na wasichana wamekuwa wakipambana kwa muda mrefu kuhakikisha sauti zao zinasikika na wana nafasi sawa katika nyanja mbalimbali za maisha yetu.

“Wanawake na wasichana ndio wahusika wakuu wa kusimamia rasilimali za maji katika jamii nyingi. Ni wao wanaotembea umbali mrefu kutafuta maji safi kwa familia zao,” amesema Jilumbi.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi.

"Kauli mbiu ya mwaka huu inatufundisha kuwa usawa wa kijinsia ni msingi wa maendeleo endelevu. Uwezeshaji wa wanawake katika sekta ya maji sio tu kwamba unaleta haki, bali pia unachangia kuboresha ustawi wa kijamii na kiuchumi wa jamii zetu. Tunapowapatia wanawake fursa ya kushiriki katika maamuzi yanayohusiana na maji, tunawapatia nafasi ya kuboresha maisha yao na ya familia zao",ameongeza.

Bi. Jilumbi amehamasisha pia umuhimu wa kutoa elimu na ujuzi kwa wanawake na wasichana ili waweze kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa maji, na kuongeza kuwa hii itawawezesha kuwa na ujuzi wa kiufundi na kuwa na uwezo wa kuchangia mawazo na suluhisho za kudumu katika sekta ya maji.

Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA pia ametumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake za kuimarisha sekta ya maji.

“Serikali imeelekeza fedha nyingi katika Mamlaka yetu kwa ajili ya miradi mikubwa inayohakikisha upatikanaji wa maji safi na salama, uchakataji wa tope kinyesi, na ujenzi wa ofisi kuu ya SHUWASA,” amesema Jilumbi.

Kwa upande mwingine, Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Bi. Nsianel Gelard, amesema uwezeshaji wa wanawake na wasichana katika sekta ya maji utaleta mabadiliko makubwa na chanya katika jamii.

"Wanawake wakiwa na nafasi sawa ya kushiriki katika maamuzi, tutakuwa na suluhisho endelevu na bora zaidi kwa changamoto zinazohusiana na maji. Pia, tutakuwa tunaboresha afya na ustawi wa jamii kwa ujumla",amesema.

Nsianel amesema maji ni uhai na ni moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu na maendeleo endelevu.

"Kwa miaka mingi, wanawake na wasichana wamekuwa wakijitolea kuhakikisha familia na jamii zao zinapata maji safi na salama. Hata hivyo, mara nyingi wamekumbana na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kijinsia, ukosefu wa elimu, na nafasi ndogo ya kushiriki katika maamuzi muhimu kuhusu maji”,ameongeza.

Akielezea kuhusu ratiba ya maadhimisho ya wanawake SHUWASA, Bi. Gelard amesema, “Sisi kama wanawake wa SHUWASA tumeanza maadhimisho haya tangu tarehe 26 Februari 2025, na tutaendelea hadi tarehe 5 Machi 2025. Katika siku hizi, tumefanya kipindi cha redio ili kuelimisha jamii juu ya shughuli mbalimbali za SHUWASA, tunaendelea kuongeza nguvu katika makusanyo ya maeneo matano ya wanawake, na kufanya usafi katika ofisi kuu.”

"Wanawake na Wasichana wa SHUWASA tunafanya kazi kwa bidii, ubunifu, uwazi, na ubora wa hali ya juu ili kuleta mafanikio chanya. Tunaungana na wanawake wote duniani kusherehekea maadhimisho haya kwa kutenda kazi zote bila kubagua",amesema Nsianel.

Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA, Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza wakati akizindua Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani 2025 kwa wanawake na Wasichana wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)

Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Bi. Nsianel Gelard akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Wanawake SHUWASA

Kaimu Mkurugenzi wa SHUWASA, Bi. Nsianel Gelard akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Wanawake SHUWASA

Mwenyekiti wa Kundi la Wanawake SHUWASA, Angel. Rweyemamu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Wanawake SHUWASA

Afisa Maendeleo ya Jamii SHUWASA, Angel Mwaipopo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Wanawake SHUWASA


Keki maalumu wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Zoezi la kukata Keki wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Zoezi la kulishana Keki wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Zoezi la kulishana Keki wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Picha wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Picha wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Picha wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Picha wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani SHUWASA

Wasichana na Wanawake SHUWASA


Wasichana na Wanawake SHUWASA








Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika ofisi kuu SHUWASA

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika ofisi kuu SHUWASA

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika ofisi kuu SHUWASA


Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika ofisi kuu SHUWASA

Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika ofisi kuu SHUWASA


Zoezi la usafi wa mazingira likiendelea katika ofisi kuu SHUWASA




Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...