Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Songwe

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira ameeleza kuwa Serikali haiwezi kueleza chochote kuhusu kuzuiliwa kwa viongozi wa upinzani kuingia nchini Angola.

Wąsira ameyasema hayo leo Mkoani Songwe alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe ambapo amesema amesoma vyombo Vya habari vikieleza kuwa kuna viongozi wa upinzani wamezuiwa kuingia Angola wakiwa katika Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo.

Viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamezuiliwa ni Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Zanzibar na Mwenyekiti wa CHADEMA.

Baada ya kuzuiliwa viongozi hao, Chama cha ACT-Wazalendo kilitoa taarifa ya kushangazwa na ukimya wa serikali kushindwa kutoa kauli yeyote huku wakiitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itoke hadharani na kufafanua kilichotokea na msimamo wa serikali juu ya hilo.

Viongozi hao, walikwenda Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD) yaliandaliwa na Taasisi ya The Brenthurst Foundation yaliyokuwa na shabaha kuwaleta pamoja wanademokrasia wa Afrika ili kutafakari kuhusu demokrasia na kubadilishana uzoefu.

Hivyo akizungumza kuhusu kuzuiliwa kwa viongozi hao Wasira amesesema amoena viongozi hao walikuwa wanaenda Angola lakini wamenyang'anywa paspoti huko Angola na sio hapa.

“Hapa hatujawanyang'anya paspoti na hata ikimaliza muda wake tunawapa, ili waende wanakotaka alafu warudi salama.Wamelalamika kwanini serikali imekaa kimya kwani sisi tunasimamia Airpoti ya Angola?

“Airpoti ya Angola inasimamiwa na watu wa Angola, na pia huenda walikuwa na jambo lao ambalo wanalilitilia shaka wangeuawa tungesema kwanini wamewaonea watu wasiokuwa na hatia," Amefafanua Wasira

Hata hivyo Wasira amesema hakuna anayejua sababu za kuzuiliwa kwa viongozi hao na huenda wametiliwa shaka labda walikuwa na jambo lao na kusisitiza Serikali haiwezi kusema chochote kwasababu tu wamezuiliwa kuingia katika nchi hiyo.”Sasa kuwaambia tu msiingie kuna tatizo gani si si mrudi tu nyumbani.”


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...