Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka, ametoa wito kwa wazazi, walimu, na watendaji wa kata kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni.

Amesisitiza kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya elimu na afya kwa watoto, hivyo ni jukumu la kila mmoja katika jamii kuhakikisha suala hilo linapewa kipaumbele na kwamba hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa kila shule ina uwezo wa kuzalisha chakula chake, hivyo kuboresha lishe ya wanafunzi na kuongeza ufanisi katika elimu.

Aidha Mhe Shaka amebainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imejipanga kutumia rasilimali zilizopo, hususani ardhi yenye rutuba, kwa ajili ya kilimo cha chakula cha shule ambapo ametoa rai kwa watendaji wa kata ambao hawana maeneo ya kilimo kutoa taarifa ili wapatiwe ardhi kwa ajili ya shughuli hiyo muhimu.

Kikao hicho kimewashirikisha watendaji wa kata zote arobaini pamoja na wataalamu mbalimbali wa sekta ya lishe na elimu, Mhe Shaka amewataka watendaji hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuweka mkazo katika suala la lishe kwa wanafunzi huku akisisitiza kuwa agizo la kuhakikisha lishe bora kwa wanafunzi ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hivyo ni lazima litekelezwe kwa vitendo.

Hata hivyo, Mhe Shaka ameahidi kuwa Wilaya ya Kilosa itaendelea kumuunga mkono Mhe Rais kwa kuhakikisha kuwa suala la lishe kwa wanafunzi linapewa kipaumbele cha juu nakusema kuwa kwa kushirikiana na wazazi, walimu, na watendaji wa kata, watahakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata chakula cha mchana shuleni, hivyo kuboresha afya na ufaulu wao.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...