Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) inashiriki katika Maonesho ya 73 ya Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI Africa) na imepata fursa ya kutembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara.
Maonyesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mount Meru Hotel, yanayofanyika sambamba na Mkutano wa 73 wa Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege – ACI Kanda ya Afrika.
Akiwa bandani, Prof. Kahyarara alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, ambaye alimueleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo katika kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini, ikiwemo maboresho ya miundombinu, usalama wa safari za anga, na kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa.
Maonesho hayo yanawaleta pamoja wadau kutoka sekta ya viwanja vya ndege ndani na nje ya Afrika, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuonesha maendeleo ya huduma za usafiri wa anga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 73 ya Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI Africa) yanayofanyika jijini Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius W. Kahyarara akizungumza jambo katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 73 ya Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI Africa) yanayofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi.

Kaimu Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano TCAA, Ally Changwila(kushoto) akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 73 ya Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (ACI Africa) yanayofanyika jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...