Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC  Nah.Mussa Mandia akizungumza na wananchi wa Mwalo wa Luhita wakati Bodi hiyo ilipofanya ziara katika Mwalohuo hawapo pichani.

Na Mwandishi Wetu

WANACNHI wa Kijiji cha Luhita, wanaotumia Ziwa la Burigi kwa shughuli za usafiri na uvuvi, wameiomba Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini (TASAC) kuchukua hatua za haraka kuondoa magugu maji yanayozidi kuenea katika ziwa hilo na kuathiri shughuli zao za kila siku.

Wito huo umetolewa wakati wa ziara ya Bodi ya TASAC walipotembelea Mwalo wa Luhita kwa lengo la kukagua hali ya usalama wa usafiri wa majini katika Ziwa Burigi. Wananchi wameeleza kuwa magugu hayo yamesababisha njia wanazotumia kusafiri na kuvua samaki kuwa nyembamba, kiasi kwamba vyombo vya usafiri majini viwili haviwezi kupishana.

Mwenyekiti wa Usimamizi wa Mazingira ya Fukwe (BMU), Nelson Atanas, amesema kuwa hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwao, hasa katika kipindi cha mvua ambapo magugu huzidi kuenea. Ameeleza kuwa ujio wa Bodi ya TASAC unatoa matumaini ya kupata msaada wa kuondoa magugu hayo na kuboresha mwalo huo kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.

Naye Leopord Baltazal, mmoja wa wananchi wa kijiji hicho, amesema ongezeko la magugu hayo linaweza kuathiri kabisa shughuli za uvuvi na kusababisha maisha kuwa magumu zaidi kwa wananchi wanaotegemea ziwa hilo kwa kipato chao.

Akijibu hoja hizo, Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC, Nahodha Mussa Mandia, amesema mamlaka hiyo imepokea changamoto hizo na itaendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha shughuli zao zinaendelea kwa ufanisi. Amesisitiza kuwa mojawapo ya hatua zitakazochukuliwa ni ujenzi wa gati na miundombinu ya msingi katika mwalo huo.

Nahodha Mandia pia alimwagiza Mtendaji wa kijiji hicho kuwasilisha maandishi rasmi ya mahitaji yao kwa Afisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Kagera, ili hatua za utekelezaji zianze kuchukuliwa. Alisisitiza umuhimu wa kuwa na vifaa vya uokozi wakati wote, kwa mujibu wa sheria za usalama wa majini.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, ikiwemo kuboresha bandari, mialo ya uvuvi na huduma za usafiri wa majini.

Mkazi wa Luhita Leopord Baltazar akitoa maelezo  kwa Bodi ya TASAC Kuhusiana changamoto ya miundombinu katika mwalo wa Luhita katika ziwa Burigi.
Mwenyekiti wa Usimamizi wa Mazingira ya Fukwe Mwalo wa Luhita Nelson Atanas akizungumza kuhusiana changamoto ya magugu katika mwalo Luhita katika Ziwa Burigi.
Wafanyakazi wa TASAC na Meneja wa Forodha Mkoa wa Kagera mwenye miwani.
Matukio  katika picha ya Bodi ya TASAC  na viongozi wa Kijiji cha Luhita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...