Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imegawa vifaa vya kielektroniki kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ngazi kata vyenye thamani ya zaidi yaTsh. Mil. 8.8 ili kuboresha utoaji huduma za maendeleo kwa wananchi hususan katika kusimamia na kuhamasisha mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sunday Deogratius amesema Vifaa hivyo vimenunuliwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo wamenunua kompyuta mpakato (laptops) za kisasa 10 pamoja na vipaza sauti 26 ambapo ugawaji wa vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa halmashauri katika kuboresha mazingira ya kazi kwa maafisa maendeleo ya jamii.

" Ninawaomba maafisa maendeleo ya jamii vifaa hivi vikawe chachu ya kuleta maendeleo kwa jamii na kuongeza ufanisi wenu wa kazi"

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Franco Mwamsyani, aliwasisitiza maafisa hao kuhakikisha wanavitumia vifaa hivyo kwa ufanisi katika kutekeleza majukumu yao. Alieleza kuwa vifaa hivyo vitasaidia katika uandaaji wa nyaraka na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu fursa za mikopo ya asilimia 10.

Grace Lupia ni miongoni mwa maafisa hao waliopokea vifaa hivyo amesema kuwa kompyuta mpakato zitawasaidia sana katika uandaaji wa nyaraka na ripoti, na hivyo kupunguza gharama na muda uliokuwa ukitumika hapo awali.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...