Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) ya nchini Tanzania na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) ya nchini Kenya zimekutana kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa udhibiti wa shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia.

Mamlaka hizo zimekutana Jijini Dar es Salaam Mei 12 na 13, 2025 na kuhusisha baadhi ya viongozi na wataalam kutoka pande zote.

Akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya Taasisi hizo, Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Mha. Charles Sangweni alisema kuwa tukio hilo ni muhimu kwa ustawi wa tasnia ya petroli nchini Tanzania na Kenya na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Tukio hili litasaidia, pamoja na mambo mengine, kuboresha ufanisi wa taasisi zetu katika kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli na kuimarisha ushiriano wa kikanda", aliongeza Sangweni.

PURA na EPRA zimebadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali yakiwemo sheria na kanuni za petroli, usimamizi wa data za petroli na mikataba ya uzalishaji na ugawanaji mapato.

Maeneo mengine ni leseni za utafutaji na uendelezaji wa mafuta na gesi asilia, na ushiriki wa wananchi katika miradi ya mafuta na gesi asilia inayotekelezwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mha. Charles Sangweni (katikati walioketi) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wataalamu kutoka PURA na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) kutoka Kenya katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha kubadilishana uzoefu baina ya Mamlaka hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mha. Charles Sangweni akitoa neno wakati wa ufunguzi wa kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya PURA na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) kutoka nchini kenya kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Biashara kutoka EPRA, Bi. Leah Jara na kushoto ni Meneja wa Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia kutoka PURA, Bw. Simon Nkenyeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...