Na Janeth Raphael MichuziTv - Bungeni -Dodoma

MBUNGE wa Kinondoni,Tarimba Abasi (CCM) amehoji ni lini Serikali itakamilisha zoezi la urasimishaji wa maeneo ya Squaters katika Jimbo la Kinondoni.

Akijibu swali hilo leo Bungeni Machi 8,2025 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophray Pinda amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Urasimishaji wa makazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Amesema hadi sasa mitaa 33 kati ya mitaa 53 ambayo ni sehemu ya mitaa 106 inayounda Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yenye majimbo mawili ya uchaguzi ya Kinondoni na Kawe imekwisha fikiwa.

Aidha amesema, makazi 60,436 yametambuliwa na kurasimishwa na Hati 11,026 zimetolewa kwa wananchi na zoezi linaendelea.

Amesema halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ni miongoni mwa Manispaa za Jiji la Dar es Salaam ambazo hadi sasa mitaa 270 katika Jiji hilo inahitaji kiasi cha shilingi bilioni 3.3 ili kukamilisha zoezi hili la Urasimishaji.

"Ni matarajio ya Wizara kukamilisha zoezi hili kadri fedha zitakavyo kuwa zinatengwa katika bajeti zetu za Wizara,"amesema Naibu Waziri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...