Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa gawio la Shilingi Bilioni 20.4 kwa Serikali kwa mwaka 2025, likiwa ni ongezeko kutoka Shilingi Bilioni 18.9 zilizotolewa mwaka 2024.

Gawio hilo limetolewa leo Ikulu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya kupokea gawio na michango kutoka kwa taasisi na mashirika ya umma. 

Vilevile, BRELA imepokea tuzo kama Taasisi iliyofanya vizuri katika kuchangia gawio kila mwaka, kwa wastani wa Shilingi Bilioni 16.8 kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi husika, wakiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya BRELA, Prof. Neema Mori, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...