•Ataja ujenzi wa hospitali ya Wilaya, miradi ya maji na ongezeko la barabara za lami.

 Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema upatikanaji wa maji Karatu Mjini ni asilimia 79, tofauti na kipindi cha miaka 25 ya nyuma ambayo maendeleo ya kusuasua jimbo hilo liliposhikiliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Amesema kutokana na hayo yanafanya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia katika rekodi ya viongozi wanaoongoza kupeleka fedha nyingi za miradi kuliko awamu nyingine yoyote tena katika kipindi cha miaka mitano.

Makalla ameeleza hayo leo Juni 5 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

“Kupitia Mkutano huu namuomba Waziri wa Maji, Juma Aweso atakuja hapa Karatu kushughulikia jambo hilo kule kwenye bwawa watakuja wanavifaa vya kutosha na uzuri tunaye waziri wa maji Kijana mwepesi na Msikivu baada ya hotuba yangu atakuja Karatu,” amesema Makalla.

Amesisitiza kuwa Aweso atakapofika katika Wilaya hiyo atashughulika na hayo mambo mawili la kwanza likiwa ni bwawa na lingine kutatua changamoto iliyopo katika kuruhusu maji ili kusaidia wananchi wa eneo hilo

Katika hatua nyingine Makalla amesema Chadema walikaa katika jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 25 na hawakuweza kuweka hospitali ya Wilaya lakini katika kipindi cha miaka michache ya uongozi wa Rais Samia Karatu wamepata hospitali ya Wilaya.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...