Na Mwandishi wetu- Karagwe

Watu 1600 wamepatiwa huduma ya matibabu ya macho wilayani KARAGWE Mkoani KAGERA huku wazee na watoto wakiwa ni waathirika wakubwa wa magonjwa hayo.

Kambi hiyo ya siku nne iliendeshwa na taasisi ya LALJI FOUNDATION kwa kushirikiana na kampuni ya Supa Foam Magodoro ambayo iliombwa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mbunge wa jimbo la Karagwe Mh. Innocent Bashungwa ililenga kutoa huduma hiyo kwa watu wenye matatizo ya macho ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu .

Akizungumza wakati wa kambi hiyo Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Karagwe Dkt. Karim Abdul amesema idadi kubwa ya watoto waliojitokeza ni wale waliorithi magonjwa hayo kutoka kwa wazazi wao tofauti na wazee ambao wengi wao wameshindwa kupata matibabu kwa wakati.

" wakazi wengi wa Wilaya ya Karagwe wanapopata maradhi ya macho wanachukua muda mrefu kwenda kupata matibabu hali inayosababisha wapate athari Zaidi za magonjwa ya macho huku wengine wakipoteza uwezo wa kuona " amesema

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Mh. Julius Laizer ameishukuru taasisi ya LALJI FOUNDATION na Supa Foam Magodoro kwa kutoa msaada huo wa kimatibabu ambao unajumuisha upimaji , upasuaji na ugawaji wa miwani kwa wananchi waliojitokeza .

" Idadi ya watu waliojotokeza kupata huduma hii inaonyesha dhahiri kuwepo kwa tatizo hili kwenye wilaya yetu na uhitaji wa huduma hii ni mkubwa na wananchi wetu wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibu hivyo tunazishukuru taasisi hizi kwa kuendesha kambi hii" amesema Mh. Laizer

Kwa upande wake mlezi wa taasisi ya LALJI FOUNDATION ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Supa Foam Magodoro Ndg. Mohsin Lalji Sheni ametoa wito kwa taasisi na watu wenye uwezo kuungana nao katika kuisaidia serikali kusogeza matibabu ya kibingwa ya macho katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema taasisi hiyo itaendelea kuweka kambi ya macho wilayani humo na wilaya nyingine za Tanzania kwasababu muitikio na uhitaji wa watu ni mkubwa hivyo zoezi hilo litakua endelevu ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Baadhi ya wananchi walionufaika na huduma hiyo wameishukuru wafadhili kwa kufanikisha zoezi hilo huku wakitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitoa kusaidia watu wenye uhitaji.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...