Na: Humphrey Shao, Michuzi Tv


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru  ndugu Ismail Ussi Leo tarehe 3 June 2025,  amezindua mradi wa Nishati Safi katika Soko la Samaki Ferry

Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa soko la samaki Feri ndugu Ismail Ussi amesisitiza umuhimu wa kuachana na matumizi ya nishati chafu kama mkaa na kuni, huku akihimiza  jamii kutumia nishati safi

“ Tumeona juhudi kubwa zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia katika kuhakikisha Watanzania wanapata nishati safi ya kupikia. Kupitia mikakati na sera madhubuti, Serikali imerahisisha upatikanaji wa gesi majumbani na kuwekeza kwenye teknolojia rafiki kwa mazingira. Hii ni ishara ya uongozi wenye maono na kujali maisha ya wananchi.”

Mradi huu umetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya Oryx Gas kwa gharama ya Shilingi milioni 216.

Mradi unalenga kupunguza matumizi ya mkaa na kuni, kulinda afya, kupunguza gharama kwa wajasiriamali, na kuhifadhi mazingira. 

“Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu “

KAULI MBIU: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”










 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...