Na Mwandishi Wetu,Chato

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira, amezuru kaburi la hayati Rais Mstaafu Dk.John Magufuli, kama moja ya ishara ya kutambua mchango wa kiongozi huyo katika kuchochea maendeleo ya taifa wakati wa uongozi wake.

Wasira ametembelea nyumba ya kudumu ya hayati Rais Magufuli leo Juni 18,2025 iliyoko Wilaya ya Chato, mkoani Geita, ukiwa ni utaratibu wa kawaida kwa viongozi wa kiserikali na kichama wanapofika wilayani hapo kutekeleza majukumu mbalimbali.

Makamu Mwenyekiti Wasira yuko mkoani Geita katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai wa chama, ambako kesho pia anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa daraja la Magufuli la Kigongo - Busisi, ambalo kwa mujibu wa taarifa za awali tukio hilo litaongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...