Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV-Katoro

MAKAMU Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ametaja mambo manne muhimu ambayo Chama kitaendelea kuyatekeleza kwa nguvu zote kwa mustakabali wa taifa.

Wasira ameyasema hayo jana Juni 17, 2025 alipokuwa akizingumza na wana CCM katika mkutano wa hadhara Katoro, mkoani Geita akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama mkoani humo ambapo pia amefanya vikao vya ndani.

Amesema jambo la kwanza ambalo CCM itaendelea kusimamia kwa nguvu zote ni umoja na mshikamano wa Watanzania ambapo alisema fafanua msingi wa umoja una mkono wa watu ambao tayari wametangulia mbele ya haki.

“Kuna wazee nyuma yetu ambao wametangulia mbele ya haki wametuachia kazi hiyo tuiendeleze, wapo wazee kama Mwalimu Julius Nyerere, Hayati Abeid Aman Karume ambaye alikubali kuacha urais wa nchi yake awe Makamu wa Rais kwa sababu ya umoja wa taifa,” amesema.

Wasira alitaja jambo la pili muhimu kwa Chama ni kusimamia amani iliyopo na kueleza kuwa sasa kuna baadhi ya watu wanachezea amani iliyopo ikiwemo kupanga kuvunja Katiba wazuie uchaguzi.

Aliwaeleza wananchi hao kuwa, yeyote anayewaambia wamuunge mkono kuchukua hatua ambazo ni kinyume na Katiba wakatae. “Ninawaambia ajenda ya amani ni ajenda yetu, tena ni ajenda ya kudumu kwa chama cha kudumu.”

Jambo la tatu alisema ni CCM kuendeleza uhuru wa taifa kwa kuwa ndio unasaidia kufanya uamuzi na kufafanua kuwa wananchi waliudai ili kuamua mambo yao wakiwa huru.

Alitaja jambo la nne ni kuendelea kuleta maendeleo ya Watanzania na katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa, nzuri kusimamia maendeleo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...