NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
KATIKA kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM imeendesha programu za mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu pamoja na uthibiti ubora wa ndani wa shule kwa viongozi wa elimu 89,716 kwa upande wa Tanzania Bara na viongozi 1,197 kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Viongozi na wasimamizi wa Elimu waliopatiwa mafunzo hayo ni Maafisa Elimu wa Mikoa, Halmashauri na Maafisa Elimu Kata. Hii imejumuisha pia walimu wakuu, wajumbe wa kamati na Bodi za shule, wathibiti ubora wa elimu na wajumbe wa Bodi za vyuo vya ualimu.
Ameyasema hayo jana Julai 9,2025 Bagamoyo mkoani Pwani Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo wakati akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwenye eneo la uongozi na usimamizi wa elimu nchini.
Amesema mafunzo hayo yalilenga kuimarisha usimamizi wa sekta ya elimu nchini ili kuendana na mabadiliko na maboresho ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 toleo la 2023.
Aidha Prof. Nombo amesema kupitia Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Elimu Msingi-BOOST, ADEM ilipatiwa kiasi cha shilingi bilioni 16,163,065,800.00 kwaajili ya utekelezaji ambapo fedha hizo zimetumika kwaajili ya kuendesha mafunzo ya walimu wakuu pia uandaaji na uchapishaji wa vitabu vya Kiongozi cha Mwalimu Mkuu "School Management Manual" na kitabu cha Utawala Bora wa Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ("LGA's Education Good Governance Manual" ).
"Vitabu hivi ni mwongozo wa Utawala Bora katika Elimu wenye kujumuisha uwekaji wa mipango ya maendeleo ya shule, usimamizi wa shule, ukaguzi wa ndani, Usimamizi wa ujenzi, ushirikishwaji wa jamii na ushughulikiaji wa malalamiko katika elimu". Amesema Prof. Nombo.
Amesema kuwa baada ya kuandaa miongozo hiyo ADEM iliendesha mafunzo ya Uongozi na Usimamizi fanisi wa shule kwa walimu wakuu 17,817 katika Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Amesema kupitia mradi huo wa BOOST, Wakala unaendelea kuendesha mafunzo ya Utawala Bora wa Elimu kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Maafisa Elimu Kata 3,956, Maafisa Elimu wa Mikoa 26 na Maafisa Elimu kutoka katika Halmashauri zote 184 nchini kwa upande wa Tanzania Bara.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...