Mkoa wa Manyara umepokea kiasi cha Shilingi Bilioni 28.499 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ambayo tayari imeanza kufanya kazi huku mingine ikiendelea na ukamilishaji wa maeneo yaliyosalia.
Fedha hizo zote zimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu nchini ili kuhakikisha Taifa linakuwa na wataalamu wabobezi katika sekta mbalimbali.
Fedha hizo zimetolewa katika awamu tatu kupitia Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ambapo mpaka sasa miundombinu ya madarasa katika shule 22 imejengwa kwa ajili ya Shule mpya za Sekondari za Kata kwa gharama ya shilingi Bilioni 11.939, Ujenzi wa Shule 2 mpya za Sekondari Mpya za AMALI kwa ghrama ya shilingi bilioni 2.184, na Ujenzi wa Miundombinu ya Shule 1 mpya za Wasichana Manyara kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.450
Miradi mingine iliyotekelezwa kupitia SEQUIP katika mkoa wa Manyara ni pamoja na Ujenzi wa Mabweni 24 kwa Shule za Sekondari kwa ajili ya Kidato cha Tano kwa gharama ya shilingi Bilioni 3.120, Ujenzi wa Vyumba 54 vya Madarasa kwa Shule za Sekondari kwa gharama ya shilingi Milioni 925, Ujenzi wa Matundu 159 ya Vyoo kwa Shule za Sekondari kwa ajili ya Kidato kwa gharama ya shilingi Milioni 228.3, Ujenzi wa Shule mpya 1 ya Sekondari ya Kanda ya Wavulana kwa gharama ya shilingi Bilioni 4.1 pamoja na Ujenzi wa nyumba 15 za Walimu kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.470
Katika Miradi hiyo ya ujenzi wa miundombinu jumla ya Shule Mpya za Kata 22 zenye vyumba vya madarasa 8 na ofisi 2, Jengo la utawala 1, Jengo la TEHAMA 1, Jengo la Maabara ya Kemia na Bailojia, Jengo la Maabara ya fizikia, Jengo la Maktaba 1, Jengo la Vyoo vya Wavulana matundu 5, Jengo la Vyoo vya Wasichana matundu 5, Kichomea taka na Tanki la Maji la ardhini zimejengwa.
Pia Mabweni 24, Vyumba vya Madarasa 54, Matundu ya Vyoo 159, Nyumba za Walimu 15, Maboma ya Maabara 05, Shule Mpya za Amali 02 (zenye Vyumba vya madarasa 8, Jengo la Utawala 1, Matundu ya Vyoo ya Wavulana 5, Matundu ya vyoo ya Wasichana 5, Mabweni 4, Bwalo 1, Nyumba ya Mwalimu 1, Chumba cha TEHAMA 1, Maktaba 1, Jengo la Maabara ya Kemia na Biolojia 1, Tanki la Maji la ardhini 1, Uwanja wa Volleyball 1, Uwanja wa Netball 1, karakana 2 na Incinerator 1).
Shule Mpya 2 (1 - Wavulana na 1 – Wasichana) zote zikiwa na Vyumba vya Madarasa 22, Maabara 3, Jengo la Utawala 1, Matundu ya Vyoo 16, Chumba cha Jenereta 1, Chumba cha TEHAMA 1, Maktaba 1, Bwalo 1, Chumba cha Wagonjwa 1, Mabweni 12, Kichomea taka 1, Nyumba za Walimu 2 (za 2in 1) na 2 za Single, Uzio na Matanki ya Maji 6.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...