Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeyataka makundi mbalimbali ya kijamii nchini kuyatumia majukwaa yao kuwahamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Wito huo umetolewa leo, tarehe 31 Julai 2025, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, wakati akifungua mkutano kati ya Tume na wawakilishi wa watu wenye ulemavu.
Katika hotuba yake, Jaji Mwambegele ameeleza kuwa Tume inatambua na kuthamini mchango wa watu wenye ulemavu katika kueneza taarifa sahihi na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi.
“Nawasihi kutumia majukwaa yenu kuhimiza wenzenu kushiriki kwa amani na kuepuka kauli au vitendo vinavyoweza kuhatarisha utulivu wa nchi yetu wakati wa kampeni,” amesema Mhe. Mwambegele, na kuongeza kuwa Tume itaendelea kushirikiana nao katika hatua zote muhimu kuelekea uchaguzi.
Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mkuu, Jaji Mwambegele amesema kuwa ratiba rasmi imeshatangazwa ambapo utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi mbalimbali utafanyika kuanzia tarehe 9 Agosti hadi 27 Agosti 2025, huku kampeni zikipangwa kuanza tarehe 28 Agosti hadi 28 Oktoba 2025 kwa upande wa Tanzania Bara.
Katika mkutano mwingine na wawakilishi wa wanawake uliofanyika pia jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Tume, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk, amewahimiza wanawake kutumia nafasi zao kuwafikishia wananchi taarifa sahihi kuhusu hatua za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, na kuhamasisha waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
Aidha, Jaji Mbarouk ametoa pongezi kwa wanawake kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha katika kipindi chote cha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kilichoanza tarehe 20 Julai 2024 na kukamilika tarehe 4 Julai 2025.
“Natoa pongezi kwenu kwa namna mlivyotuunga mkono wakati wote wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Tunawapongeza na tunawashukuru sana,” alisema Jaji Mbarouk.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Tume, Mheshimiwa Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari, amewahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa uadilifu, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi.
“Natoa wito kwenu kuwahamasisha vijana kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na kuepuka mitandao inayosambaza habari za chuki na uchochezi,” amesema Jaji Asina.
Ameonya pia dhidi ya matumizi mabaya ya teknolojia ya akiliunde (AI), ambayo kwa sasa inatumika kusambaza taarifa za upotoshaji na chuki.
“Vilevile, muwakumbushe vijana wenzenu kuepuka matumizi mabaya ya akiliunde. Vijana ni kundi lenye nguvu, na mkitambua nafasi yenu, mtaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” aliongeza.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...