Mwanasiasa na mwalimu kitaaluma, Mosses Mdaka Mapunda, ni mtia nia nafasi ya Udiwani katika Kata ya Masumuni, Wilaya ya Mbinga, Mkoa wa Ruvuma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), akiahidi kuleta mwelekeo mpya wa maendeleo ya kweli katika kata hiyo.

Mapunda anaamini kuwa Kata ya Masumuni inahitaji kiongozi aliye karibu na wananchi, mwenye uelewa wa changamoto zao, na aliye tayari kushughulikia matatizo yao kwa vitendo. Anasema anafahamu kiu ya wananchi wa Masumuni kwa maendeleo na ana dhamira ya dhati ya kuhakikisha matarajio yao yanatimia kwa vitendo.

Mosses Mapunda alianza kushiriki siasa rasmi mwaka 2010 akiwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tangu wakati huo amekuwa akihudumu ndani ya chama katika nafasi mbalimbali kwa uadilifu na kujituma.

Mwaka 2015, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Masumuni, nafasi aliyohudumu hadi mwaka 2020. Hadi sasa, ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, nafasi anayoshikilia kwa kipindi cha 2023 hadi 2027.

Katika kipindi chote cha utumishi wake ndani ya chama, Mapunda ameonyesha kuwa ni kiongozi mwenye maono, msikivu, mchapakazi, na mwenye uwezo mkubwa wa kushirikiana na wananchi katika kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.


ELIMU NA TAALUMA.


Mapunda ni mzaliwa wa Bonde la Hagate, Kata ya Mapera, Wilaya ya Mbinga. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kiwanjani iliyopo Mbinga Mjini. Elimu ya sekondari aliipata katika Shule ya Sekondari St. Paul’s, ambayo sasa ipo Wilaya ya Nyasa, Baada ya hapo alijiunga na Chuo cha Ualimu Mtwara Kawaida ambapo alipata stashahada ya ualimu, na baadaye alihitimu shahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Kwa zaidi ya miongo miwili, Mapunda amehudumu kama mwalimu na mhamasishaji wa maendeleo katika jamii. Elimu yake, taaluma yake, na uzoefu wake katika sekta ya elimu vinampa msingi madhubuti wa kusimamia masuala ya kijamii kwa weledi.

MCHANGO KWA JAMII.

Tangu mwaka 2010, Mosses Mapunda amekuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya Kata ya Masumuni na kata jirani. Baadhi ya michango yake ni pamoja na Kutoa mashine za kuchapisha (photocopy) kwa shule na ofisi za kijamii, Kuchangia fedha za ujenzi wa zahanati katika maeneo ya kata,
Kusaidia ujenzi wa ofisi ya chama cha siasa.

Amekuwa akitoa misaada kwa jumuiya za kijamii zikiwemo za vijana na wanawake, Kushiriki kikamilifu katika harambee za maendeleo ya elimu na afya Mapunda ameweka rekodi ya kuwa mdau wa maendeleo asiyechoka, akijitolea kwa vitendo pasipo kusukumwa, kwa nia ya dhati ya kuona maisha ya wananchi yanabadilika.


DIRA YA MAENDELEO KWA MASUMUNI

Kwa mujibu wa Mapunda, nia yake ya kugombea udiwani si kwa ajili ya heshima binafsi, bali ni matokeo ya maono na wito wa kuwatumikia wananchi wa Masumuni kwa moyo wake wote.

Dira yake inajikita katika maeneo makuu ambayo ni Kuboresha elimu kwa kujenga na kukarabati miundombinu ya shule, kuongeza vifaa vya kujifunzia na kuhimiza ushiriki wa jamii katika kuinua elimu ya mtoto wa Masumuni, Kuboreshwa kwa huduma za afya kwa kuhakikisha zahanati na vituo vya afya vinapata vifaa na dawa kwa wakati, pamoja na upatikanaji wa wahudumu wa kutosha.

Amelenga Uimarishaji wa miundombinu ya barabara, maji na umeme katika vijiji na mitaa ili kufungua fursa za kiuchumi na kijamii, Kuwawezesha vijana na wanawake kiuchumi kwa kusimamia miradi ya ujasiriamali, vikundi vya mikopo na kutoa elimu ya stadi za maisha, Uwajibikaji wa viongozi na usimamizi wa fedha za umma kwa kuhakikisha rasilimali za serikali ya mtaa zinatumika ipasavyo, kwa uwazi na kwa manufaa ya wananchi wote.


WITO KWA WANANCHI NA WANACHAMA WA CCM.


Mosses Mdaka Mapunda anatoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi wote wa Kata ya Masumuni kumpa nafasi ya kuwa Diwani wao katika uchaguzi ujao, Anaahidi kuwa kiongozi wa kusikiliza, kushirikiana na kushughulikia kero zao kwa ufanisi na kwa wakati.

Kwa uzoefu wake wa kisiasa, elimu yake ya kitaaluma, na moyo wake wa kizalendo, Mapunda anaamini kuwa Masumuni inaweza kuwa mfano wa kata yenye maendeleo endapo atapewa ridhaa ya uongozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...