Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo kikuu cha Dar-esslaam Dkt Juma Mohamed Matindana,ni miongoni mwa wanachama wa Chama hicho waliochukua fomu kwa ajili ya kuwania kugombea Ubunge katika Jimbo la Tunduru Kaskazini Mkoani Ruvuma kupitia Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza  jana kwenye ofisi za Chama  cha Mapinduzi Matindana alisema,nia yake kubwa ni kuwa sauti ya wananchi wa Tunduru hasa wale wa kawaida ambao watashirikiana kutatua changamoto zilizopo katika jimbo la Tunduru Kaskazini.

Kwa mujibu wa Dkt Matindana ni kwamba, yeye ni Mwanachama wa chama cha Mapinduzi kuanzia mwaka 2003 na amekuwa kiongozi wa Chama hicho kama mjumbe wa Halmashauri kuu Wilaya na mlezi wa kata mbalimbali za kichama.

Alisema, kwa sasa ameona ni muda mfuaka yeye kurudi nyumbani kama mwakilishi wa Wananchi kwenye nafasi ya Mbunge kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.

Amewaomba wanachama wa Chama hicho kumuunga mkono katika harakati za kugombea Ubunge wa Jimbo  hilo na kuhaidi kuwa iwapo atateuliwa na kuchaguliwa atashirikiana na wananchi pamoja na Chama cha Mapinduzi kusukuma maendeleo.

Wakati huo huo Mfanyabiashara maarufu Wilayani Tunduru Boniface Chacha Marwa, ni miongoni mwa wanachama waliojitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea ubunge katika Jimbo la Tunduru Kaskazini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Chacha alisema,amejitafakari na kujiridhisha kwamba ana uwezo wa kugombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini na kwa kushirikiana na wananchi atahakikisha Jimbo hilo linapiga hatua kubwa kimaendeleo na kiuchumi.

Alisema,iwapo Chama cha Mapinduzi kitampa ridhaa na wananchi kumchagua kuwa Mbunge wao watalibadili Jimbo la Tunduru Kaskazini kuwa kitovu cha kiuchumi kutokana na uwepo wa rasilimali kubwa za madini na ardhi inayofaa kwa kilimo cha mazao ya kila aina.

Naye Kada wa Chama hicho Ziada Matewele ni miongoni mwa wanachama wa Chama hicho waliochukua fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Tunduru kusini.

Alisema, katika jimbo la Tunduru kusini kuna kero kubwa  hususani wananchi kukosa soko la uhakika la kuuza mazao yao na kupitia yeye na Serikali watatua changamoto za wananchi wa Jimbo hilo.

Amekiomba Chama cha Mapinduzi kumpa kipaumbele wakati utakapofika kwa kuchagua yeye kama mgombea mwanamke kugombea Ubunge katika Jimbo hilo.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Tunduru Yusuf Mabena alisema,zoezi  la kuchukua fomu linaendelea vizuri na jumla ya wanachama 15 wakiwemo wanawake 4 wamejitokeza kuchukua fomu.

Alisema,kwa upande wa Jimbo la Tunduru Kaskazini waliochukua fomu ni wananchama 6 na  jimbo la Tunduru Kusini wamejitokeza wanachama 9.

Mabena alisema,kwa upande wa nafasi ya udiwani jumla ya wanachama 128 wamejitokeza kuchukua  kwa ajili ya kuomba ridhaa ya Chama hicho kugombea udiwani kwenye kata mbalimbali.

Amewataka wanachama wenye sifa,kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuchaguliwa na Chama kwenye nafasi ya Udiwani na Ubunge.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...