KATIKA kutekeleza mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha barabara za mijini na vijijini vinapitika wakati wote, Wilaya ya Kaliua imetekeleza mkakati huo kwa vitendo.

Katika kuthibitisha hilo, Mbio za Mwenge wa Uhuru umezindua mtambo wa kutengeneza barabara (Motor Grader) wenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambao utatumika kwenye shughuli za ujenzi na ukarabati wa barabara katika wilaya hiyo iliyopo mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dk. Gerald Mongela, amesema mtambo huo utawezesha barabara za wilaya hiyo kupitika katika kipindi chote.

"Kama unavyofahamu wilaya yetu idadi kubwa ya wananchi wake wanajishughulisha na kilimo, hivyo mtambo huu utafungua barabara hadi zile za mashambani kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao hususan tumbaku bila kikwazo," amesema Dk. Mongella.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...