Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) linashiriki katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na watakuwepo hapo kipindi chote cha maonesho ili kuwawezesha Watanzania.

Akifafanua hilo Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza Bi. Minaeli Kilimba ameeleza kuwa wamekuja kuwaelezea watanzania juu ya Mifuko ya Uezeshaji na namna wanavyoweza kunufaika nayo na kuutarifu Umma fursa zinazopatikana katika Mifuko hiyo.

Sambamba na hilo ameeleza kuwa wamekuja sabasaba kuvitangaza vituo vya uwezeshaji takribani 28 vinavyopatikana nchini ma huduma za kiuwezeshaji zinazopatikana latila vituo husika. 'Niwaombe watanzania watembelee banda la Ofisi ya Waziri Mkuu na kufika lilipo Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ili kuweza kupata taarifa za kiuwezeshaji kiundani zaidi' aliongeza Bi. Minaeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...