Na Said Mwishehe,Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ametoa rai kwa vyama vya siasa nchini kuzingatia Dira 2050 wanapotoa Ilani zao.
Akizungumza leo Julai 8,2025 jijini Dar es Salaam mbele ya wahariri na waandishi wa habari ,Profesa Mkumbo amesema kuwa mchakato wa Dira 2050 imehusisha watanzania wa makundi mbalimbali na miongoni kupitia vyama vya siasa.
“Vyama vya siasa 19 vimeshiriki kikamalifu,vyama vikubwa na vidogo vyote vimepata nafasi.Tulimuomba Msajili wa vyama vya siasa atuaandalie mkutano na vyama vya siasa wametoa maoni yao.
“Tumekubaliana kwenda safari moja ya Dira 2050 ya Tanzania Tuitakayo . Hivyo wanasiasa hatutabishana kuhusu dira ya maendeleo ila watapishana wanatumia usafiri gani kuifikia hiyo dira.
“Vyama vya siasa wamekubaliana kuweka Ilani inayoakisi Dira 2050 na hata ccm Ilani yetu tumezingatia dira hiyo Hivyo tunatarajia na vyama vingine vya siasa Ilani zao zitaangalia dira 2050.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...