Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa amani na kuhubiri masuala ya amani na utulivu wa Nchi ili kuepuka madhara yatokanayo na uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu

Akizungumza leo jijini Dar es salaam latika kikao maalum na viongozi wa Dini RC Chalamila amesema viongozi wa dini ni muhimili katika kutunza amani ya nchi huku akisisitiza kuwa serikali kupitia jeshi la polisi itaendelea kuimarisha ulinzi na amewataka watanzania kujifunza madhara ya uvunjifu wa amani kupitia mataifa jirani yenye vurugu

Aidha RC Chalamila ameongeza kuwa hakuna kiongozi anaependa kuona wananchi wake wakikabiliwa na vitendo vya ukatili na uvunjifu wa amani hivyo ni muhimu kwa viongozi wa Dini kusimama imara kupitia madhabahu kwenye nyumba za ibada kuhubiri amani

Kwa upande wa Shekh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya amani ya Mkoa huo Shekh Walid Kawambwa amesema viongozi wa Dini wana nafasi kubwa ya kuimarisha amani na kujenga maadili ndani ya jamii hivyo watumie nafasi zao vizuri huku Mtume Boniface Mwamposa wa makanisa ya Arise and Shine akihimiza viongozi wa Dini kutumia vyema madhabahu kuhubiri amani

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo amesema kuwa viongozi wa dini wamekuwa na mchango mkubwa katika kuombea amani na utulivu wa nchi kwa kushirikiana na makundi mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara na bodaboda.









 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...