Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa bandari kavu ,Kwala iliyopo Wilaya ya Kibaha utakaofanyika tarehe 31 ,2025 (kesho) umekamilika.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari leo tarehe 30 2025 uliofanyika Bandari Kavu Kwala Mkoani hapa amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa 95.

"Mgeni rasmi atakua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Mikoa jirani wajitokeze kwa wingi kwa sababu jambo hilo ni la kihistoria ndani na nje ya nchi" amesema RC Kunenge.

Kunenge ameongeza kwa kusema kuwa sambamba na uzinduzi wa bandari kavu pia Rais Dkt. Samia atazindua Kongani ya viwanda ya Kwala ambayo ona uwezo wa kuwa na viwanda 250.

"Eneo la Kwala ni sehemu ambayo serikali imefanya uwekezaji mkubwa ikiwa pamoja na ujenzi wa viwanda vikubwa 250 ambapo hadi sasa tayari viwanja saba tayari vimejengwa na vinafanya kazi.

"Bandari Kavu ya Kwala ina uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku na Makasha 30,000 kwa mwaka.

Kunenge amesema bandari kavu ya Kwala itaongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ambapo kimsingi bandari imelenga kusaidia na kupunguza msongamano wa makasha katika bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 30.

RC Kunenge amesema kuwa Dkt. Rais Samia siku hiyo atazindua maeneo ya ujenzi wa bandari kavu kwa ajili ya nchi za DRC Kongo, Zambia, Burundi, Malawi, Zimbabwe na Uganda ambapo pia amesema kuwa nchi za Sudan na Somalia nao wameonesha nia ya kujenga bandari kavu katika eneo hilo.

Wakati huohuo Rais Dkt. Samia atapokea mabehewa 160 ya reli ya kati ambapo kati ya hayo mabehewa 20 yamekarabatiwa na mabehewa 100 yamenunuliwa mapya na serikali na mengine 40 yamekarabatiwa na Shirika la Chakula Duniani pamoja na Wakala wa Ushoroba wa Kati.

RC Kunenge amesema kuwa Rais Dkt.Samia ataweka jiwe la msingi kwenye Kongani ya Viwanda ya Kwala yenye viwanda 250 Kongani ambayo ni kubwa katika nchi yaKuhusu Bandari Kavu ya Kwala, Kunenge amesema mradi huo ,utaongeza ufanisi mkubwa kwa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku sawa na zaidi ya makasha 300,000 kwa mwaka hatua itakayopunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya asilimia 30.

Aidha RC Kunenge amesema kuwa Rais Samia anatarajiwa kupokea jumla ya mabehewa 160 ambapo mabehewa 100 ni mapya yaliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya reli ya MGR ,mabehewa 20 yamefanyiwa ukarabati na mabehewa 40 yametolewa na WFP.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...