Na: Calvin Gwabara – Dar es salaam.

Watanzania wametakiwa kutambua kuwa miswada ya sheria haitoki serikalini pekee bali hata wananchi wanaweza anzisha mchakato na kupendekeza mswada wa sheria wanayoitaka kutungwa kupitia wawakilishi wao bungeni.

Mwandishi wa Sheria kutoka OCPD Bwana Vincent Masalu (Wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Jumanne Abdalah Sagini

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Jumanne Abdalah Sagini wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara SABASABA yanayoendelea jijini Dar es salaam ambayo Ofisi hiyo inashiriki kwa lengo la kutoa elimu ya masuala mbalimbali ya uandishi wa sheria, ufasili wa sheria pamoja na urekebu.

“Kumekuwa na dhana kuwa miswada yote ya sheria inaanzishwa na Serikali na hivyo kuwafanya wananchi kuona kama wanatungiwa sheria tu na serikali bungeni kitu ambacho sio sahihi kwani wananchi popote walipo nchini wanaweza kuanzisha mchakato wa kutengeneza mswada wa sheria na kisha kuuwasilisha bungeni kupitia wabunge wao” Alifafanua Mhe.Sagini.

Aliongeza “Niwaombe nyinyi kama wataalamu kutoka Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kutumia nafasi ya uwepo wenu kwenye maonesho haya makubwa kuwapatia wananchi elimu ya kina kuhusu mchakato wa uandaaji wa miswada maana maonesho haya yanawaleta watu wa makundi mbalimbali ambao wakipata elimu hiyo wataifikisha kwenye jamii zao na hivyo kuongeza uelewa kwa jamii yetu”.

Aidha Naibu huyo wa Wizara ya Katiba na Sheria ameipongeza Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa kukamilisha kufanya urekebu na kutoa toleo la mwaka 2023 lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi wanne mwaka huu na ambalo limeanza kutumika tarehe 1 mwezi wa 7 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga ambaye ametembelea banda hilo la OCPD kwenye maonesho hayo ameipongeza Ofisi hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kufanya urekebu wa sheria kuu zote nchini.

Hata hivyo Jaji huyo ametaka kujua kuhusu kanuni za sheria hizo zilizofanyiwa urekebu kama pia zipo tayari kwaajili ya matumizi na baada ya kupata majibu ameiomba Ofisi hiyo pamoja na majukumu mengi waliyonayo ameshauri kuzikamilisha mapema ili nazo ziweze kupatakana kwa wakati ameishauri ofisi hiyo kuhakikisha zinakamilika.

Kwa upande wake Mwandishi wa Sheria kutoka OCPD Bwana Vincent Masalu akitoa maelezo na ufafanuzi kwa viongozi hao amesema tayari Ofisi inaendelea na zoezi la kufanyia kazi kanuni za sheria hizo ili kuhakikisha zinakwenda sambamba na sheria kuu.

Masalu amesema wataalamu wa Ofisi hiyo wanafanya kazi usiku na mchana kushughulikia mambo yote bila kuchoka ikiwemo zoezi la ufasili wa sheria kuu zote ambazo zinatarajiwa kutolewa mwezi wa nane na hivyo kusadia jamii kupata sheria na kanuni zake.

“Tunatumia fursa ya kuwepo kwenye  maonesho haya ya sabasaba kuwafikia wadau wengi zaidi kwakuwa kwenye maonesho haya kuna wadau wote wa sheria kuanzia Wananchi wa kawaida, Taasisi za kiserikali na Wizara na hivyo kuwa sehemu muhimu ya kuwafikia wadau wetu na kuwapa elimu ya masuala ya kisheria kwa maana ya mchakato wa utungwaji hadi kusainiwa na Mhe. Rais kuwa sheria pamoja kuwaelewesha majukumu yanayotekelezwa na Ofisi yetu ya Mwandishi Mkuu wa Sheria” alifafanua Masalu.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga akisisitiza jambo kwa Waandishi wa sheria katika banda ya Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Mwandishi wa Sheria kutoka OCPD Bwana Vincent Masalu akifafanua jambo kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga.


Mwandishi wa Sheria kutoka OCPD Bwana Vincent Masalu akimkabidhi zawadi Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga.



Mwandishi wa Sheria kutoka OCPD Bwana Vincent Masalu akimkabidhi zawadi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Jumanne Abdalah Sagini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...