NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, amesema kuwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji wa huduma za bima yanatarajiwa kuongeza kiwango cha wananchi wanaotumia bima ya afya kutoka asilimia 37 mwaka 2025 hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Dkt. Saqware ameyasema hayo leo katika Maadhimisho ya Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama “Saba Saba,” wakati akizungumza katika Kijiji cha Bima kilichopo katika viwanja vya maonesho.

Amesema Kijiji cha Bima kinajumuisha zaidi ya watoa huduma 30 wa bima, ambao wanatoa huduma mbalimbali kwa wananchi wakiwemo wale wanaohitaji bima ya afya.

Aidha, amewahimiza wananchi kutembelea kijiji hicho ili kupata huduma hizo muhimu kabla ya maonesho kufikia tamati tarehe 13 Julai 2025.

"Kijiji chetu kina msimamizi ambaye atakupa utaratibu wa kupata leseni ya bima, kupokea malalamiko mbalimbali, na pia kutoa elimu ya bima kwa lengo la kulinda haki za wateja," amesema Dkt. Saqware.

Vilevile, amebainisha kuwa kuungana kwa kampuni zaidi ya sita za bima, zikiwemo NHIF, katika kuanzisha Kijiji cha Bima ni hatua ya utekelezaji wa Sheria mpya ya Bima ya Afya, ambayo ilianza rasmi kutekelezwa kuanzia Julai 1, 2025.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...