Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Energetech-Tantel zimetiliana saini Hati ya Makubaliano (MOU) itakayowezesha usindikaji na usambazaji wa gesi asilia nchini kote.
Utiaji saini wa tukio hilo la kihistoria, ulishuhudiwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati nchini Tanzania Bw. Goodluck Shirima, akiwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dk. Doto Biteko.
Utiaji saini huo unakwenda sanjari na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuifanya Tanzania kama kituo kikuu cha nishati kikanda,ikiwamo Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
MOU inaeleza mpango kazi kabambe wa miaka miwili unaojumuisha tafiti , vibali muhimu, uhandisi wa kina, upatikanaji wa fedha, na hatimaye, uzalishaji wa kimiminika cha gesi( LNG). Uzalishaji wa kwanza wa LNG unatarajiwa ndani ya miezi 12 ijayo.
Mradi huu bunifu unalenga kutumia rasilimali za gesi asilia za Tanzania na kuzifanya zipatikane kwa urahisi na kwa wingi kwa watumiaji wa nishati ili waweze kuwa na nishati safi.
Mradi huo, unaokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 80–100, kwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa mtambo wa LNG wa kisasa utakaobadili gesi kuwa kimiminika ili iweze kusafirishwa katika mitungi maalumu.
Uzalishaji wa awali unakadiriwa kuwa kati ya futi za ujazo milioni 20 hadi 30 (scf) kwa siku, na uwezo mkubwa wa kupanuka zaidi ya futi za ujazo milioni 100, kukidhi mahitaji ya nishati yanayokua.
Chini ya masharti ya mkataba huo, Energetech-Tantel itaongoza vipengele vya ufadhili, uhandisi, na usambazaji wa bidhaa za mwisho wa mradi, ikilenga kutoa nishati mahali panapohitajika zaidi.
Aidha TPDC itatoa msaada muhimu katika upelekaji wa gesi kwa ajili ya kusindikwa na kuwa kiungo cha ushirikiano na mamlaka za serikali, ikiwa ni pamoja na taratibu muhimu za vibali.
Bw. Goodluck Shirima, Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati Tanzania, alisema baada ya utiaji saini akizungumza na waandishi wa habari kuwa: "Uwekezaji wa sekta binafsi ni muhimu kwa kutoa suluhisho zinazoweza kutumika kuendeleza viwanda kwa Tanzania, kipaumbele kikiwa kuendeleza matumizi ya ndani ya gesi . Mara baada ya kuanza kazi, kaya na viwanda vya Tanzania vitafaidika na nishati safi ya gesi, na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji."
Naye Mkurugenzi Mtendaji, TPDC Bw. Mussa Makame alisema :"Katika TPDC, tunashabikia ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi unaotoa suluhisho kwa Watanzania,"
Aidha alisema kwamba mkataba huo umelenga kutumia rasilimali kuwezesha nishati safi na kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika na nchi za jirani pia.
“Tunajivunia kushirikiana na Energetech-Tantel katika uzalishaji wa gesi kwani ni muhimu kwa mkakati wetu."
Afisa Mtendaji Mkuu wa Energetech-Tantel. Bw. Alistair Naiken alisema kuwa mktaba huo sio wa ushirikiano tu ushirikiano, bali ni ahadi ya pamoja ya kubadilisha sekta ya nishati Tanzania.
"Tunajenga suluhisho za nishati halisi ambazo zitabadilisha jamii, tukitoa gesi mahali na kwa wakati tgukiipeleka inapohitajika zaidi, huku lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati hii kwanza, hasa wateja wa viwandani, kama nishati safi ."
Rais na COO, Tantel Holdings,Bw. Daniel Gabai, akitoa maoni yake amesema: "Tanzania ni nchi yenye matumaini zaidi Afrika Mashariki. Katika Tantel Holdings, hatuwekezi tu katika uwezekano bali katika watu, tukikumbatia changamoto kubwa za miundombinu.
“Tunaamini Tanzania itakuwa nguvu inayoongoza kwa ukuaji barani Afrika katika muongo ujao, na mradi huu utakuwa mradi bora zaidi wa nishati safi barani, ukiwahudumia soko la ndani na kikanda."
"Upatikanaji wa suluhisho za nishati ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote," alihitimisha Bw. Moshe Schlisser, Mwenyekiti, Tantel Holdings.
"Kupitia ushirikiano huu, tunatarajia kutoa nishati inayoweza kupanuka na endelevu, kuiweka Tanzania kama kiongozi katika nishati mbadala Afrika Mashariki. Mradi huu utatoa ajira za moja kwa moja kwa maelfu ya Watanzania na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuendesha ukuaji wa viwanda, kuifanya Tanzania kuwa kituo cha nishati safi Afrika."

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...