WADAU Wadau wa Kilimo katika mnyororo mzima wa thamani wameshauriwa kuchangamkia fursa za kijasiriliamali na kibiashara zilizopo katika sekta ya Kilimo kwa kutumia Teknolojia zilizofanyiwa Utafiti zinazolenga kuongeza tija ya Mazao na kipato kwa mtu Mmoja na taifa kwa Ujumla.

Wito huo umetolewa Julai 06, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Thomas Bwana katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Bwana amesema lengo la Tafiti zinazofanyika ni kuhakikisha zinazoongeza kipato kwa wadau wa Kilimo katika mnyororo mzima wa thamani kuanzia kwa Mkulima hadi msindikaji.

"Furaha yetu Watafiti ni kuona wakulima na wadau mbalimbali wanapata fedha kwa matumizi ya teknolojia zilizobuniwa na watafiti ambazo zinachangia kupunguza gharama za uzalishaji huku tija ikiongezeka bila kusahau wasindikaji ambao kimsingi sio lazima wawe ni Wakulima " Amesema Dkt. Bwana.

Kutokana na hilo Dkt. Bwana amesema katika Maonesho haya n TARI imekuja na bidhaa mbalimbali zilizoongezewa thamani kama vile unga wa mchicha, biskuti za unga wa Muhogo, Unga lishe wa Maharage na nyingine nyingi ili kutoa elimu ya fursa za kijasiriliamali iliyopo katika kilimo sekta ya Kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...