Na CHRISTOPHER LISSA

WATAALAMU wa majengo katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajia kukutana Zanzibar katika kongamano maalumu la kujadili teknolojia ya ujenzi kuanzia mwaka 1960 hadi 2025.

Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Wabunifu Majengo Tanzania (AAT) .

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, Rais wa AAT, Mbunifu Majengo, Meck T’Chawi amesema, kongamano hilo litafanyika kuanzia Julai 10 hadi 11 mwaka huu katika Hoteli ya Maadinat Al Bahr Zanzibar.

“Ni tukio kubwa litakalokusanya wabunifu majengo , wahandidsi na waadiriaji majenzi kutoka nchi zote za Afrika Mashariki,”ameelezaa T’Chawi.

Amebainisha, kongamano litajikita kujadili kukua kwa teknolojia ya ujenzi tangu mwaka 1860 hadi mwaka huu.

“Tuta jadili kwa kina kuhusu uli za ujenzi hasa a majengo ya kale yaliyojengwa na waarabu, wajerumani na waingereza. Zanzibar ina majengo mengi ya namna hiyo,”amesema.

Amedai, dhamira ni kuwaonesha wananchi wan chi za Jumuiya EAC kuhusu ukuaji wa teknolojia katika majenzi na jinsi ya kuhifadhi majengo hayo.

Rais T’Chawi, amewataka wananchi kuhuduhuria kwa wingi katika kongamano hilo kwani litatumika kubadilisha ujuzi na taaluma ya teknolojia ya ujenzi katika nchini za EAC

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wabunifu Majengo Afrika Mashariki, Attie Ahmed Ally, alisema, waliichagua Zanzibar kwa lengo la kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kukuza utalii.

“Zanzibar ni mji wa kitalii. Una majengo mengi ya kale.Tuyaangalia kiundani majengo haya kujua kutoka 1860 mpaka sasa teknolojia yetu ya ujenzi imekua kwa kiwango gani,”ameeleza Attie

Amesema, kongamano hilo litaambatana na maonesho makubwa ya vifaa vya ujenzi ambapo wananchi watapewa elimu namna ya kutumia vifaa bora

Katibu wa AAT, Mbunifu Majengo Naroka Njau, amesema kongamano hilo pia litajikita kujua utamaduni ulipotoka na ulipo.

“Utamaduni wa wakoloni na jinsi ulivyoungana na utamaduni wa Tanzania na kadri unavyo badilika.

Utamaduni hii unapoendelea kubadilika ndivyo teknolojia ya majengo inavyo kua,”amebainisha Naroka.

Mjumbe wa Kamati ya AAT Mbunifu Majengo, Mbaraka Igangula, alisema kongamano hilo litakuwa tukio kubwa na lenye kuleta tija katika sekta ya ujenzi.

“Sera yetu inaelekeza makazi bora kuanzia mijini hadi vijijini. Kongamano hili litatupa tathimini wapi makazi bora yalianza na yalipofika. Tunawaomba vijana walioko katika vyuo kujumuika ili kukutana wakongwe wa ujenzi kutoka Afrika Mashariki. Hii ni fursa,”amedai Igangula.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...