Na Mwandishi Wetu

MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kwilasa Deogratias ambaye alikuwa mmoja wa watia nia ya Ubunge katika Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza amekishukuru Chama chake kwa hatua waliyofikia baada ya kura ya maoni sasa wanaenda kupata wagombea kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba.

Akizungumza jijini Mwanza leo Agosti 5 mwaka huu Deogratias amesema amekuwa mwanachama mwaminifu tangu mwaka 2012 na mwaka 2015 alipata nafasi ya kura za maoni katika Jimbo la Magu na mwaka 2020 jimbo la Ukerewe.

Ameongeza mwaka huu 2025 alikuwa mmoja wa watia nia katika jimbo la Nyamagana jijini Mwanza na hivyo anakishukuru chama chake cha CCM kwa hatua waliyofikia baada ya kura za maoni wanaenda kupata wagombea wa chama hicho katika kila jimbo.

“Ahadi yangu ni kuwa mwanachama na kada mwaminifu ili kwenda kuhakisha chama chetu kinapata ushindi wa kishindo na ili tuweze kupata viongozi bora wanaweza kutafasiri ilani ya chama chetu kwa vitendo.

“Nashukuru chama chetu kwa kufanya utaratibu wa kupata wagombea kwa haki na uwazi,naamini itatupa tumaini na ushindi mkubwa.Asante sana viongozi wa wilaya ,mkoa hadi taifa ya kusimamia jambo hili vyema.

“Tuko tayari kushirikiana na madiwani ,wabunge na rais (wateule wa chama chetu)kufanya kampeni ,mtaa kwa mtaa,kila sehemu kuhakikisha ushindi unapatikana,CCM hoyee,kidumu Chama Cha Mapinduzi,kazi na utu tunasonga mbele,asanteni sana.

Aidha amesema rai yake kwa Wana CCM huu muda wa kuvunja makundi sio muda wa kurusha vijembe na kwamba enzi za mchakato ilitokea habari inayotaka kufanana na hii vijembe vingi baadae wakanyamaza.

“Tujitahidi kutunza furaha zetu na wenye maumivu wajitahidi kuweka ustahimilivu ili tuungane kwa ajili ya kukipambania chama …mapambano yanayofuata sio ya mtu tena bali ni mapambano ya chama kwanza mtu baadae ..ukiwa comred kwenye siasa Kuna Raha yake.”



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...