MGOMBEA wa nafasi ya udiwani wa Kata ya Kisutu, wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, Tousif Bhojani, amechukua fomu za uteuzi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na kueleza kuwa dhamira yaya ni kuijenga Kisutu mpya.
Bhojani alichukua fomu leo katika Ofisi za Ofisa Mtendaji Kata ya Kisutu, ambapo alikabidhiwa fomu hizo na Ofisa Mtendaji Kata hiyo Joyce Mambo.
“Ninashukuru CCM Kisutu kwa kuniamini na kunipitisha kuwania nafasi hii. Leo nimechukua fomu hii kuipeperusha bendera ya Chama katika kata yetu. Nitaijaza na kuirejesha. Wakati utakapofika ninawaomba wananchi wa kisutu kunichagua na kura nyingi kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.Mitano tena,”ameeleza Bhojani.
Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Kisutu, Murtazar Darugar, aliwataka wananchi katika kata hiyo kumpa ushirikiano mkubwa Bhojani.
“Tumpe ushirikiano. Tumpe ushirikiano Rais Dk. Samia kwa kura nyingi za kishindo. Kisutu mpya inakuja,”alisema Daruger.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa kata hiyo, Edith Temu, alisema Bojani anatosha kuiongoza kata hiyo na watasimama naye kidete kuhakikisha CCM inashinda na Rais Dk. Samia anapata kura nyingi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...